SERIKALI BORESHENI MASLAHI YA WATUMISHI KUZUIA UFISADI

 

📌JASMINE SHAMWEPU.

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU na aliyekuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utoh amesema ili kutokomeza ufisadi serikali na Taasisi binafsi zinatakiwa kuangalia na kuboresha maslahi ya watumishi wao.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Taasisi za Umma na Binafsi kuweza kudhibiti ufisadi katika maeneo yao.

Ni ukweli kuwa mishahara ya watumishi ni midogo na mtumishi anayeishi maisha ya kawaida akisema aishi kulingana na mshahara huo bila kujishughulisha lazima mtu atafute njia za mkato ili kufanikisha na kutunza familia inayomtegemea,

Serikali iangalie upya mishahara ya watumishi wakati mwingine watu au watumishi wanalazimika kuvunja sheria na kujiingiza katika vitendo vya rushwa kutokana na Maslahi. 

Mkurugenzi Utouh

Aidha amesema katika nchi ya Tanzania Ufisadi upo na Rushwa ipo ambapo ameeleza jambo hilo limekuwa likiitesa dunia kwani ufisadi unaumiza uchumi wa nchi na kuchelewesha maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Kwa upande wake Ancletus Mhidze kutoka Idara ya ukaguzi wa ndani daraja la kwanza akimuwakilisha Mkaguzi Mkuu wa Serikali amesema ufisadi umekuwa ukitokea katika miradi mikubwa ya kimaendeleo na wakaguzi wa ndani wameonekana kutofanya kazi zao ipasavyo hii ni kutokana na ufinyu wa bajeti na vitendea kazi.

Naiomba serikali kuwepo na bajeti ili wakaguzi wa ndani waweze kufanya kazi zao ipasavyo na kuweza kufichua na kuzuia mambo ya rushwa kwani vitengo vya ukaguzi wa ndani bajeti ni ndogo.

Naye Shakibu Mussa Nsekela bingwa katika masuala ya Ubadhilifu, Kudhibiti Rushwa na Ufisadi amesema Madeni hewa yanachangia kwa kiasi kikubwa ufisadi Tanzania na ili kuweza kusonga mbele wanaopewa nafasi ya kusimamia watu na miradi watende haki  kwenye miradi,  fedha zitumike na miradi ionekane.

Hata hivyo amesema madeni hewa yataweza kuondolewa kwa wananchi kwa kuongeza uwazi, uaminifu na uadilifu kwa watumishi wa umma pale wanapokuwa wanasimamia malipo au wanapotoa malipo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments