RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji
la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3 huku akieleza namna anavyoisikia sauti
ya mtangulizi wake hayati Dkt.John Magufuli akimtaka kuendeleza miradi mingine
yote aliyoiacha.
Rais Samia amesema atahakikisha anaiendeleza miradi
yote iliyoachwa na Dk. Magufuli na kuwataka wananchi kuitunza.
Kauli hiyo ameitoa Leo Februari 9,2022 wakati
Akizungumza katika ghafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa arabara ya
mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma (km 112.3).
Rais Samia amesema siku ya leo toka asubuhi anasikia
sauti ya mtangulizi wake ikimueleza kuhusu miradi aliyoiacha ikiwemo ya kuhamia
Dodoma na mingine ikiwemo huu wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma.
Ndugu zangu siku kama ya leo mimi mwenzenu toka asubuhi nasikia sauti ya mtangulizi wangu Dkt John Pombe Magufuli ananiambia kuhusu miradi hii, kuhusu Dodoma kuwa makao makuu, kuhusu mambo mengi,
Na leo hii tupo hapa kuweka jiwe la msingi la mradi huu lakini kàzi hii waswahili wanasema ukiona vinaelea vimeundwa na kwa bahati nzuri muundaji wa suala hili aliyetekeleza maono ya taifa kuhamia Dodoma akataka kuipanga Dodoma kwa bahati mbaya hatunaye,Mungu amemchukua,
Lakini ameniachia urithi mzito nami niahidi mawazo yote aliyoyaanzisha nitakwenda kuyatekeleza kikamilifu. Leo hii ni moja kati ya mawazo aliyoyaanzisha niahidi pamoja na kuungwa mkono na African Bank tunaenda kukamilisha mradi huu kama alivyotaka Magufuli
Rais Samia.
Katika hatua nyingine Rais amesema Serikali inatumia
fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1
ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua
masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa
mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.
Ndugu zangu Benk kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benki kwa ajili ya waafrika
Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga barabara
23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.
Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya tano kuleta vuguvugu hili pamoja na kuungwa mkono na Benki ya Maendeleo na hawapo katika barabara wapo pia katika maji na umeme tumewaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu
Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo,Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi
Rogatus Mativila amesema lengo la kujenga barabara hiyo ni kupunguza
msongamano katika Jiji la Dodoma.
Amesema jumla ya gharama ya Mradi huo ni shilingi
bilioni 249 ambazo ni kwa ajili ya fidia na ujenzi ambapo amedai kuna miradi
midogo midogo kama ujenzi wa vituo vya afya,ununuzi wa ambulance wakati wa
utekelezaji wa mradi huo.
Mtendaji huyo wa TANROADS ameeleza kuwa lengo ni
kupunguza msongomano mkubwa wa magari katika Mkoa wa Dodoma ambao
ungesababishwa na muingiliano wa magari yanayosafiri kupitia mjini.
Ameeleza kuwa barabara hiyo ina umbali wa Km 20 kutoka
katikati ya Jiji la Dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni
M/s AVIC INTL Project na China Civil Engineering Construction Cooperation zote
kutoka Jamhuri ya watu wa China.
Alifafanua kuwa
awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba
na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu
na Nala.
Kwa upande wake,Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika(AFDB) Dk.Akinwumi Adesina amesema wataendelea kushirikiana na Serikali
ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amedai wanaamini
Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji.
Amesema Benki hiyo imewekeza kwa kutoa fedha kwa ajili
ya miradi mbalimbali yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 2.5.
Miaka kadhaa iliyopita nilikaa na kuzungumza na rafiki yangu,mtu wa watu hayati Dk.Magufuli kuhusu kutekeleza mradi huu ,Kwa bahati mbaya hayupo tena lakini Kutokana na ushirikiano wake kwetu tunaahidi kuendelea kishirikina na watanzania kwa miradi mingi zaidi.
Naye,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame
Mbarawa amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa Kujenga barabara hiyo kutokana
na ongezeko la watu pamoja na Dodoma kuwa Makao Makuu hivyo magari yanayoingia
na kutoka kuwa mengi.
Tunatoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kutekeleza mradi huu,imetoa fedha nyingi katika miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya wakandarasi
Bila kuwa na Mahusiano mazuri hili lisingetokea niipongeze Wizara kwa mradi huu mkubwa ni ubunifu mkubwa na utafungua fursa nyingi hivyo.
Mwisho.
1 Comments
Casino Roll
ReplyDeleteJoin Casino goyangfc.com Roll dental implants Online wooricasinos.info Casino Roll septcasino 2021 바카라 사이트