📌RHODA SIMBA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa
serikali ya Mkoa itawasomesha wanafunzi 43 wa kidato cha tano na sita kwa
waliofanya vizuri kidato cha nne 2021 kwa shule za serikali.
Kadhalika Mtaka amenunua alama "A" kwa
shilingi 5000 lengo likiwa ni kuwapa motisha walimu wa masomo ambayo wamepata
alama hiyo na kila mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza ya pointi 7 hadi
9 kwa wanawake na kwa wanaume pointi 9, serikali ya Mkoa itawalipia ada.
Ameyasema hayo Jijini hapa katika hafla ya utoaji tuzo
kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri matokeo ya kidato cha nne 2021, ambapo
amesema kuwa watagharamia, vifaa vya shule pamoja na kulipa kwa kipindi cha
miaka miwili.
Amefafanua kuwa wanafunzi hao 43 (wasichana 35 na
wavulana 8) kutoka shule za sekondari za Mpwapwa,Lukundo,Mlowa barabarani,
Dodoma, Msalato girls, Mtera Dam na Gode
Gode.
Mtaka amesema wanataka wawe na ushindani kwenye uchumi
hivyo lazima wawekeze katika suala la elimu kwani hakuna nchi duniani
iliyoendelea bila kuwekeza katika elimu.
Kazi ya serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi hawa ni kuwezesha na kuhakikisha ada na vifaa vinapatikana, wajibu wa mzazi utabaki katika suala la sare za shule, mzazi mtoto wako akipangiwa shule njoo na barua yake tuletee sisi tunampatia vifaa pamoja na kulipa ada. Na leo tunawapatia madaftari 9 kila mmoja
Mtaka.
Kamati ya kitaalamu tuone namna ya kufanya mitihani ya
mara kwa mara ya vitendo na kama mzazi anauwezo wa kumuwezesha mtoto wake
atafute mwalimu amuwezeshe kwani sifuri atakayoipata haita nizuia, haitamzuia
afisa elimu kula itabaki kwenye familia yako,' amesema.
RC Mtaka akikabidhi vyeti kwa baadhi ya walimu ambao shule zao zimefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2021 |
Aidha amewataka maafisa elimu kuwapa heshima, kuwatunza walimu na kuwasifia pale wanapostahili sifa.
Na nyie wanafunzi mnao wajibu wa kusoma kila matokeo ni ya wanafunzi na wazazi wao hivyo mjitahidi kusoma
Mtaka.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa Fatma Mganga amesema kuwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni 900 na kwamba inaashiria kuwa wameanza safari ya sekta ya elimu kwenda kufanya makubwa.
0 Comments