NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema, Serikali inathamini na kuheshimu nafasi ya watoto na vijana katika kuchangia maendeleo ya Taifa.
Mpanju ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha kukusanya maoni kutoka kwa watoto yatakayoingizwa kwenye mtaala mpya wa Elimu utakaotumika katika shule za msingi, sekondari na elimu ya ufundi nchini.
Hatuwezi kuongelea maendeleo ya kiuchumi, Sayansi na Teknolojia, siasa na utawala na mfumo nzima wa Mila na Tamaduni pasipo kushirikisha vijana wetuMpanju
Ameongeza kuwa, katika mchakato wa kupitia mtaala uliopo na kuandaa mtaala mpya ni muhimuTaifa kupanga mipango ya Maendeleo ikishirikisha vijana.
Katika hili nisisitize matakwa ya Sheria za nchi hususani Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 imeelekeza bayana kuwashikirikisha watoto na vijana katika shughuli zote za KitaifaMpanju.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu Mpanju, amemuelekeza Kamishna wa Ustawi wa Jamii kusimamia uundwaji wa mabaraza ya watoto nchi nzima ili watoto wayatumie kama majukwaa ya kujadiliana masuala yanayohusu.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto Sebastian Kitiku akieleza lengo la kikao hicho amesema, watoto wameshiriki kwa sababu mtaala ni suala linalowahusu, hivyo maoni yao ni lazima yatajumuishwa na kuzingatiwa katika mtaala huo.
Katika Sera yetu ya Mtoto ya mwaka 2008 ina maeneo makubwa matano, ambayo moja ya eneo ni kuwashirikisha watoto katika masuala yanayowahusu, jambo la kupitia mitaala wa Elimu ni kubwa Kwa watoto na vijanaKitiku.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya TET Dkt. Aneth Komba amesema, zoezi hilo ni muhimu sana na tangu April 2021 TET imeanza mchakato wa kufanya mapitio ya mitaala na tayari wadau mbalimbali wameshapata maoni yao katika kuboresha.
Amesema katika mtaala wa sasa ilionekana hauwawezeshi wahitimu wengi fursa ya kujiajiri na kuajiriwa au kumudu maisha ya kila siku hivyo ilifanya Taasisi hiyo kupitia na kufanya maboresho.
Wakiwasilisha sehemu ya maoni yao baadhi ya vijana walioshiriki kikao hicho wameshauri mtaala ulenge kuwapa Stadi za kuwawezesha kumudu changamoto za maisha ya kila siku.
Kikao hicho cha siku mbili kwa lengo la kuhakikisha mtaala
utakaoandaliwa uendane na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yaliyopo sasa
na umehudhuriwa na wawakilishi wa watoto na vijana 26 kutoka Mikoa yote
Tanzania Bara, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
0 Comments