📌JOYCE KASIKI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (EWURA) imetaja Bei mpya za mafuta aina ya petrol dizel na
mafuta ya taa kwa mwezi februari mwaka huu ambapo baadhi ya mikoa imepanda na
mikoa mingine kupungua.
Aidha ,kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa
bei ya mafuta kwa mwezi Machi na Aprili 2022.
Hayo yamesemwa leo Februar Mosi 2022 na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati Akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kupandia na kushuka kwa bidhaa hizo kwa baadhi ya
mikoa nchini.
Ameswma Bei za rejareja za mafuta ya
petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es
Salaam,zimepungua kwa shilingi 21 kwa Lita (petroli) na shilingi 44 kwa Lita
(mafuta ya taa) wakati Bei ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 13 kwa Lita.
Aidha alisema Bei za reja reja kwa mafuta ya
petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga,Kilimanjaro,Arusha na
Manyara)zimepungua kwa shilingi 123 kwa Lita (petroli) na shilingi 92 kwa Lita
(dezeli mtawalia)huku akisema kutokana na kumalizia kwa mafuta ya taa kwenye
maghala ya kuhifadhia yaliyopo Tanga .
Amewataka waendeshaji wa vituo vya mafuta
kwenye mikoa ya Kaskazini kuchukua mafuta ya taa kutoka Bandari ya Dar es
salaam ili Bei za mafuta ya taa katika mikoa hiyo zilingane na gharama za kupokelea
mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka
mikoa husika.
Mhandisi Chibulunje amesema Bei za rejareja za
mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kusaini (Mtwara,Lindi na Ruvuma)
zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa January 5 mwaka huu huku akisema hiyo ni
kwa sababu mwezi January hakuna shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia Bandari
ya Mtwara.
Vile vile Mhandisi huyo amesema kwa kuwa
hakuna maghala ya kuhifadhia mafuta ya taa katika Bandari ya Mtwara,waendeshaji
wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusaini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa
kutoka katika Bandari ya Dar es salaam ili Bei za rejareja za mafuta ya taa
ilingane na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam
na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.
Mhandisi Chibulunje amesema,katika kuhakikisha
kunakuwa na ushindani sawa katika Bei zinazoanza kutumika februuari 2,2022
,ununuaji wa mafuta kutoka kwenye maghala Sasa kutakuwa na Bei mbili yaani Bei
kikomo ambayo muuzaji hatatakiwa kuzidisha na Bei ya chini ambayo muuzaji
hatatakiwa kushuka zaidi.
Akizungumzia mwendo wa bei za mafuta kwa mwezi
Machi na April mwaka huu amesema,upo uwezekano wa bidhaa hiyo kuongezeka katika
soko la dunia.
Hata hivyo amesema Ewura inaendelea kufuatilia
mwendo huo kwa karibu ili kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika harakati
za kupunguza makali ya Bei za mafuta katika kipindi hicho.
0 Comments