📌RHODA SIMBA
Hayo yamesemwa
hii leo jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Godfrey Chibulunje wakati
akitangaza bei mpya itakayoanza kutumika hapo kesho februari 2 ambapo
amesema mafuta ya petrol yamepungua kwa shilingi 21 kwa lita, mafuta taa
shilingi 44 kwa lita na dizeli imepanda kwa shilingi 13 kwa lita.
Bei za rejareja kwa mafuta ya petrol na dizeli kwa mikoa ya kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimepungua kwa shilingi 123 kwa lita petro na shilingi 92 kwa lita kwa dizeli mtawalia
“Kutokana na
kumalizika kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya kuhifadhia yaliyopo
Tanga waendeshaji wa vituo vya mafuta katika kanda ya kaskazini
wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya dar es salaam na
hivyo bei za rejareja katika mitaa hiyo itakuwa kulingana na gharama za
kupokelea” amesema Chibulunje.
Amesema bei za
reja reja za mafuta ya petrol na dizeli kwa mikoa ya kusini Mtwara Lindi na
Ruvuma zitaendelea zile zile zilizotangazwa katika toleo la tarehe 05 january
2022 hii ni kwasababu kwa mwezi January hakuna shehena ya mafuta iliyopokelewa
kupitia bandari ya Mtwara.
Pia kwa kuwa hakuna maghala ya kuhifadhi mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara waendeshaji wa mafuta wa mikoa ya kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es salaam na hivyo bei za reja reja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kwa kutumia bandari ya Dar es salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika
0 Comments