📌WMJJWM- DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ameongoza shughuli ya mazishi ya Kijana Egidi Gangata, aliyechomwa kisu na kijana mwenzie wa mtaani wakati kijana huyo akijaribu kupigania haki za vijana wadogo waishio mitaani jijini Dodoma,
Akiwa katika shughuli hiyo ya mazishi, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa jamii kuongeza elimu ya malezi kwa watoto, ili kuepusha jamii kuacha watoto kukimbilia mitaani ambapo hukumbana na kadhia kadha wa kadha ambazo huwasababishia kupoteza Maisha kama ilivyotokea kwa Kijana Egidi na hivyo kupoteza ndoto zao.
Tukio hili la kusikitisha la kijana Egidi, linatufundisha kuwa ndoto za watoto wengi zinapotea tangu wakiwa watoto kwa kujikuta wameingia kwenye mkondo hasi wa mfumo wa maisha hususan maisha ya mitaani na kuacha kuishi ndani ya familia ambazo mwisho wa siku huangukia kwenye madhila kama haya
Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima amesema, tukumbuke kuwa, maisha ya mtaani yanawafundisha watoto mambo mengi mabaya na ya uovu, na kwamba kama taifa hatuwezi kuwa na jamii salama kama tukizungukwa na watoto wasio na fursa za makuzi mema ya huko mitaani, kwani, matokeo yake hata pale serikali au wadau wanapotaka kuwapa maisha mapya wanatupilia mbali fursa hiyo. Hii siyo sawa, amesisitiza Dkt. Gwajima.
Akitoa Mahubiri katika Ibada yakuwafariji wafiwa, Mchungaji na mlezi wa Egidi, kiroho, amesema mara zote kijana huyo, alikuwa na tabia njema na kifo chake kimetokea wakati akipigania haki za watoto wadogo waishio mitaani ambao miongoni mwao walikuwa wananyang’anyana pesa, walizo jipatia baada ya kuomba kwa watu mitaani.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Jiji la Dodoma Rebbeca Ndaki, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji hilo, alisema, kilichotokea kwa kijana huyo ni matokeo ya Jamii, kujitenga na watoto wao wakati wa makuzi, hivyo tunaiomba jamii iwe bega kwa bega na watoto na kutaka kila mzazi kutimiza wajibu wake.
Katika mazishi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na katibu Kata wa CCM wa Kata hiyo ya Kikuyu, Wesu Rajabu, alisema kifo hicho kinasikitisha kwakuwa, inashangaza kuona familia ambazo Pamoja na kuwa na uwezo lakini zimeshindwa kuchukua nafasi yake ya malezi na makuzi kwa viajana wao.
Haya Matukio sasa yanazidi kila mara kwani, juma lililopita tulimzika kijana mwingine ambaye kifo chake kilitokana na mazingira yanayofanana sana na haya yaliyo mkuta Egidi ni wito wangu sasa tubadilike tabia.Wesu Rajabu.
Mwaka 2017/18 Serikali ilizindua Mpango Kazi wa Kupambana na Ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambao umeelekeza kuundwa kwa Kamati za Mapambano kuanzia Kitongoji, Mtaa, Kijiji, Halmashauri, Mkoa na Taifa hiyo rai ya Waziri Gwajima ikawa ni kuzitaka kamati hizo kuamka na kutekeleza wajibu wao.
0 Comments