WAZIRI BASHUNGWA AELEKEZA MACHO KWENYE BIMA YA WAFANYABIASHARA WADOGO

 


ANGELA MSIMBILA-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe kutoka NBC na Britam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya bima ya wafanyabiashara wadogo.

Waziri Bashungwa amekutana na NBC ofisini kwake Jijini Dodoma na kuwapongeza  Benki hiyo na  Britam kwa kufanya utafiti wa kina katika masuala ya bima kwa wafanyabiashara.

Amemuelekeza Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa akiambatana na ujumbe wa NBC na Britam kuungana na timu inayoendelea na uchunguzi wa kufungua kwa soko la Karume ili kuwa na majadiliano ya kuhusu bima.


 

Waziri Bashungwa  amewashauri NBC na Britam kwa kushirikiana na Serikali, kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu Elimu ya Bima na kuwashauri timu hiyo kuwashirikisha Mamlaka ya Bima Tanzania TIRA katika Kamati hiyo.

Katika Kikao hicho  Mkuu wa kitengo cha Bima kutoka NBC  Bw. Benjamin Nkaka alielezea kuwa, Benki  hiyo ilishafanya uchambuzi katika kuwapatia bima wafanyabiashara wadogo (wamachinga) pindi yanapotokea majanga kama moto, mafuriko.

Nkaka ameelezea kuwa, mitaji kwa wafanyabiasha wadogo ni kati ya elfu 50,000 hadi 100,000,000. Kutokana na mitaji hiyo, ada ya bima kwa kila mfanyabiashara kwa mwaka ni kati ya shilingi 25,000 hadi 295,000. Hata hivyo katika kuongeza mtaji kwenye bima, NBC wamekuwa wakishirikiana na Britam kuhakikisha wanawafikia wafanyabiashara wengi.

Post a Comment

0 Comments