📌 MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso mwishoni mwa wiki amemteua Afisa Habari na Uhusiano wa Malaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma Mjini (DUWASA) Sebastian Warioba kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi,kituo atapangiwa baadaye.
Warioba ambaye pia ni Mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma amewashukuru wadau mbalimbali kwa kumpa ushirikiano katika yake.
Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na afya njema. Utukufu ni wake yeye Mungu wetu. Pili, nimshukuru sana Waziri wetu wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) na Uongozi mzima wa Wizara ya Maji kwa Imani yao kwangu.Ameandika Warioba katika walaka wake wa kutoa shukrani kwa wadau mbalimbali baada ya kupata taarifa za uteuzi huo.
Niwashukuru Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri ya Jiji hususani Wahe. Madiwani, Wahe. Wenyeviti, Watendaji wa Kata na Mitaa na Mabalozi kwa namna tulivyoshirikiana kuijenga DUWASA na pale palipohitaji maboresho mlitoa michango yenu kwa dhati za mioyo yenu!Warioba amesema anatambua na kukiri mchango wa wana tasnia ya Habari kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake katika kitengo cha Habari na Uhusiano ndani ya DUWASA
Naye Mwenyekiti wa CPC Mussa Yusuph amempongeza Warioba kwa uteuzi huo huku akimsihi kwenda kuchapa kazi ili kulipa Imani ya Waziri Aweso katika jukumu hilo la kusimamia mamlaka ya maji atakayopangiwa.
Tunampongeza sana ndugu Warioba,alichokifanya Waziri Aweso ni muendelezo wa Imani kubwa inayooneshwa na Serikali kwa wana tasnia ya Habari,hivyo tunapopewa nafasi hizo twende tukawaoneshe kwamba wapo sahihi kutukabidhi nafasi hizo kwa kutekeleza majukumu yetu kwa weledi ili kuhudumia wananchiMussa Yusuph
Katika kutambua mchango wa Bw.Warioba katika tasnia ya Habari mkoani Dodoma,mwezi Mei mwaka 2021 katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,CPC ilimpa tuzo kwa mchango wake mkubwa ndani ya klabu.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt.Selemani Serera (Kushoto) akimkabidhi tuzo Sebastian Warioba,hii ilikuwa mwaka 2021. |
0 Comments