📌RHODA SIMBA
MJUMBE wa halmashauri Kuu CCM Wilaya ya Mkinga na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Baraza la UVCCM Mkoa wa Tanga Hamis Rajabu (35) amejitosa kuchukua fomu ya Kugombea nafasi ya Uspika.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoka kuchukua fomu ya kugombea uspika amesema kuwa ana haki ya kuwa spika na kuonesha Umma kuwa vijana wanaweza kuongoza Bunge.
Amesema kuwa tangu Bunge limeanzishwa mwaka 1956 alijawahi kuongozwa na Spika kijana na sasa umefika wakati wa kuongozwa na kijana.
Amesema kuwa umefa wakati sasa wa vijana kushika nafasi kubwa za maamuzi badala ya kudhani kuwa wanaotakiwa kuongoza ni wazee tu.
Katika hatua nyingine Mgombea Uspika,Rajabu amesema iwapo chama kitampitisha kugombea nafasi hiyo na kuwa Spika hatahakikisha anawafundisha wabunge jinsi ya kuchangia.
Amesema wakati wa mijadala na kuchangia kiti cha Spika kitaelekeza bunge kazi za wabunge,Naibu Mawaziri na Mawaziri na namna ya kuikosoa serikali na kuishauri serikali.
Amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anarudisha Bunge katika dira ya kibunge na kufuata sheria zenye kuhakikisha mhimili wa Bunge unafanya kazi kwa ukamilifu.
Aidha amesema kuwa katika uongozi wake wa kuliongoza Bunge hatahakikisha kila jambo ndani ya Bunge sheria,Kanuni na misingi yote inaendelea kwa kufuatia misingi.
"Kuna mikataba ambayo inaingizwa ndani ya Bunge ambayo inaingia buneni kwa hati ya dharura na kutokana na hiyo inatakiwa kuangaliwa vizuri.
" Bunge linatakiwa kuwa la wananchi kwa kutoa usawa kwa watu wote bila kuwa na ubaguzi wa aina yoyoye kwa lengo la kutenda haki kwa watu wote"amesema Rajabu.
0 Comments