📌DODOMA.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema atawapa kazi maalum aliyekuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais Samia , ametoa kauli hiyo leo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, wakati akiwaapisha viongozi wateule aliowateua hivi karibuni,ambapo amesema kutokuwepo kwenye orodha ya baraza jipya la mawaziri haimanisha kuwa amewaacha.
Mkiwatazama hawa umri wao kama wangu na ukitizama niliyowateua hamfanani kabisa. kwahiyo kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu ili waje wanisaidie wanisimamie kuwasimamia nyie . kwahiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo orodha ni kwasababu hapo wote wadogo wadogo na mnahitaji kusimamiwa vizuri ,kwahiyo wawili wale watakuja kwangu tuwasimaie nyinyi
Aidha, amesema Profesa Kabudi amefanya kazi kubwa ya kusimamia mazungumzo ya serikali na mashirika na ndio kazi ambayo anataka kumkabidhi .
‘’ Aendelee na kazi hiyo ila kazi yake kwasababu haipo kwenye muundo haitangazwi wala nini , lakini atasimamia hiyo kazi ,kazi zote zitakazo ingia na serikali kabudi ataongoza hiyo timu,kaka yangu yeye anakazi na mimi nitamvuta baadae lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia ninyi’’ amesema Rais
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema yapo majukumu mengi kwenye kila sekta na kila mmoja kwa nafasi yake ni muhimu kwenda kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.
‘’ Tutafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu na kufanya kazi kwa matokeo chanya. Kwenye mipango na majukumu yetu tutafanya kazi kwa matokeo chanya kwa kuwatumikia wananchi na kuwasilikiliza kule walipo’’ amesema Majaliwa
Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Akson amewataka viongozi hao kwenda kumsaidia Rais na wanapokwenda kutejeleza majukumu yao wafanya kama wasaidizi wa Rais huku Jaji wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma akisema amewataka kwenda na kiapo cha ujaji kwa kuzingatia katiba na sheria ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama.
0 Comments