📌RHODA SIMBA
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi anatarajiwa kufanya uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria utakaofanyika tarehe 23 January mwaka huu Jijini Dodoma.
Sherehe hizo za uzinduzi zitaanza kwa zoezi la matembezi yatakayoanza saa12:00 asubuhi katika viwanja vya kituo jumuishi Cha haki Jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa hii leo January 21 jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka a ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema matembezi yataanzia viwanja vya kituo Jumuishi Cha haki(Jengo jipya la mahakama karibu na hazina) na kuishia kwenye viwanja vya Nyerere square ambapo sherehe za uzinduzi zitafanyika.
Aidha amezitaka taasisi zote za Serikali,binafsi,makundi mbalimbali,wadau wote wa mahakama na wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya wiki ya Sheria kitaifa.
Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na jirani mjitokeze kwa wingi katika maadhimisho ya wiki ya Sheria kitaifa(January 23-29,2022) na siku ya Sheria nchini (February 1,2022)kuungana na viongozi wetu Mhe.Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania,Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muhimili wetu wa Mahakama
Mkuu wa Mkoa.
Amesema maadhimisho ya wiki ya Sheria yatafanyika kwa wiki nzima yakijumuisha shughuli uzinduzi wa bendera ya mahakama(Januari 23,22),uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ya chemba (Januari 25,2022),uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la makao makuu ya mahakama ya tanzania-judicial square (Januari 26,2022) na Uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ya bahi(January 28,2022).
Kwa upande wake, Naibu Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma, Bernard Mpepo amesema kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na uzinduzi wa majarida na sheria mbalimbali zinazohusu mahakama zitakazofanywa na jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Pia, amesema Januari 23, kutakuwa na uzinduzi wa bendera ya mahakama, Januari 25 uzinduzi wa mahakama ya wilaya ya Chemba, Januari 26 uwekaji jiwe la msingi la mradi wa jengo la makao makuu ya mahakama ya Tanzania na Januari 28 uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ua Bahi.
Sherehe za maadhimisho ya wiki ya Sheria kitaifa zitafanyika kwenye mkoa wa Dodoma makao makuu ya Nchi kuanzia tarehe 23 Januari mwaka huu hadi 29 Januari mwaka huu Aidha sherehe za siku ya Sheria nchini zitafanyika pia kwenye makao makuu tarehe 01 februari mwaka huu.
Pia sherehe za siku ya Sheria nchini zitakazofanyika katika viwanja vya bustani ya chinangali (februari 1,2022) Mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments