HABARI PICHA:WAZIRI MHAGAMA ALIVYOPOKELEWA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
January 10, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Watumishi wa
Ofisi yake mara baada ya kuripoti rasmi baada ya kuapishwa na Mhe. Rais
kuiongoza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kulia
kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye
kabla alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikabidhiwa ofisi na mtangulizi
wake Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya kuapishwa rasmi leo na Mhe. Rais
kuiongoza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe.
Mchengerwa kwa sasa ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed
Mchengerwa akitoa neno la shukrani kabla ya kukabidhi ofisi kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama leo jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Post a Comment
0
Comments
Hey there, We are Blossom Themes! We are trying to provide you the new way to look and use the blogger templates. Our designers are working hard and pushing the boundaries of possibilities to widen the horizon of the regular templates and provide high quality blogger templates to all hardworking bloggers!
0 Comments