MTAKA AWATAKA 'MACHINGA KUWA WAAMINIFU

 


📌RHODA SIMBA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthon Mtaka amewataka viongozi wa soko jipya linalojengwa jijini hapa Machinga Complex kuhakikisha wanazingatia  uaminifu na kubaini wanaojisajili zaidi ya mara moja jambo ambalo halitavumilika na wataondolewa eneo la Mradi.

Ameyasema hayo leo Januari 13 jijini hapa  mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa soko la Machinga Complex,mradi utakaotumia zaidi ya 7b/- na unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Machi 17 mwaka huu,ambapo litakuwa soko la kisasa litakalo zingatia huduma zote za kijamii ikiwemo sehemu ya akina mama kunyonyesha watoto.

Inapofika tarehe 17 machi mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan tunataka tumzawadie Machinga Complex,na tunataka iwe machinga ambayo itawaweka wa machinga wote na iwe machinga ya kisasa na taarifa zake zote ikiwemo kitambulisho

Mtaka

Nae Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema kuwa mradi huo una uwezo wa kuwa mudu watu zaidi ya elfu tatu mpaka  elfu 5 ambapo zoezi la kusajili  linaendelea kwa njia ya kielektroniki na kwamba soko hilo likimalizika litasaidia Dodoma kuwa safi bila kukuta mtu barabarani kama sasa hivi .

Tunatarajia zoezi likishakamilika  hapata kuwa na machinga barabarani ambae anauza bidhaa zake na jiji letu litakaa katika hali ya usafi niseme tu ukweli hatutamfumbia macho mtu ambae ataendelea kukaa barabarani

Mafuru

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara Bruno Mponzi amewataka wamachinga kuwa wazalendo huku wakidai kwamba endapo watabaini mmoja wao anashiriki udanganyifu atachukuliwa hatua.

Nae meneja wa eneo hilo la Mradi Mohamed Jafari amemhakikishia Mkuu wa Mkoa na uongozi wote hukakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati.

 

Post a Comment

0 Comments