📌JOYCE KASIKI
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdullah amezindua mradi wa kutengeneza maabara yay a Akili Bandia (Robott)kwa maendeleo ya Afrika (AI4D) wenye lengo la kuzifundisha mashine ili ziweze kufanya kazi zinazofanywa na mwanadamu.
Akizungumza wakati akizundua mradio huo Abdullah alisema,mradi huo umekuja wakati muafaka ambao nchi inatakiwa kidigitali huku akisema kwa Afrika itakuwa ni maabara ya pili kwa kuwa na teknolojia hiyo wezeshi .
Teknlojia hii inakwenda kugusa mambo mengi yakiwemo kilimo ,afya …,na ukiangalia sasa hivi nchi yetu inakwenda kwenye ulimwengu wa kidigitali na serikali ya awamu ya sita imeweka mkazo mkubwa sana kwenye eneo hilo,kwa hiyo kuwa na teknlojia hiyo itasaidia kuwa na ‘transformation ‘ya nchi yetu kwenye hilo.
Awali Kiongozi wa Mradi huo kutoka UDOM Dkt.Ally Nyamawe amesema, mradi huo una nguzo tatu ikiwemo kufanya tafiti,kufanya mafunzo na kufanya bunifu ambapo kila nguzo ina aina yake ya watu watakaowachukua ili kupata watu watakaokuja na mawazo mazuri ya kibunifu yanayoenda kutatuamatatizo katika sekta mbalimbali .
Dkt.Ally alisema,Mradi huo unatarajiwa kukamilika kipindi cha miaka miwili na nusu ambapo umelenga kufundisha mashine ili ziweze kufanya kazi ambazo zinafanywa na mwanadamu kwa kutumia akili.
“Kwa mfano labda kwenye afya tunataka tujue mgonjwa ameathirika na ugonjwa gani kwa hiyo unaweza ukachukua picha za exray ukaingiza kwenye mashine na mashine ikautambua ugonjwa husika.”amesema Dkt.Ally
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga alisema,ni mradi mkubwa wa kisayansi ambao matokeo yake lazima yatakuja kusaidia maendeleo ya nchi.
“Sasa hivi katika nchi yetu tunaelekea kwenye uchumi wa kidigitali lakini pia tunaelekea kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda,haya yote hayawezi kutekelezeka bila mapinduzi kwenye eneo la tehama”amesema na kuongeza kuwa
Kwa hiyo leo tunapopata nafasi ya kufungua huu mradi wa Akili Bandia(Robott) ambao ni moja kati ya teknolojia ya juu sana katika matumizi ya tehama ambayo huleta mapinduzi ya viwanda na katika sekta zote za maendeleo .
Hata hivyo Profesa Luoga amesema,licha ya kuwa tgeknolojia hiyo inakwenda kuleta changamoto kwenye suala la ajira lakini pia inapaswa kuifanya nchi ianze kubadilika hasa katika suala la mitaala kwamba kuanzia shule za msingi watoto waanze kufundishwa matumizi ya teknolojia .
“Kwa hiyo hii tuichukulie kama fursa kuelekea kwenye nchi ya kidigitali ambayo itatufanya wote tuelekee kwenye fursa ya kubadili mifumo yetu ya elimu ili baadaye wote wajue umuhimu wa matumizi ya tehama.”
0 Comments