📌RHODA SIMBA
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Dr.Linda Peniel Salekwa amejitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya kuwa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akisema kuwa ataitendea haki nafasi hiyo endepo atapendekezwa.
Dkt.Selekwa amechukua fomu hiyo leo jijini hapa katika ofisi kuu za CCM Dodoma na ameelezea dhamira yake ya kuwania nafasi hiyo kuwa ni kutimiza takwa la kikatiba la chama chake na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiahidi kuisaidia Serikali kutimiza malengo yake kupitia Mhimili wa Bunge.
Ameongeza kuwa kilichomshawishi zaidi kujitosa katika nafasi hiyo ya uspika ni hamasa aliyoipata kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amewataka vijana kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zinazotokea za uongozi.
Mimi kama kijana nitakuwa bega kwa bega na Serikali ya Rais Samia ambaye amekuwa akiwaunga mkono vijana na mbali na mimi kuwa Mhadhiri nmekuwa nikihamasisha vijana hasa wakike Katika maswala ya Sayansi pamoja na uongozi
Pamoja na hayo Dkt.Salekwa amesema kuwa kwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya uspika wa binge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kwa vitendo na kuwa mfano kwa vijana wa kike na kuwaonesha kuwa hata vijana hasa wa kike wana haki na wajibu wa kuwania nafasi kubwa serikali.
Hata hivyo ikumbukwe kwamba zoezi la uchukuaji fomu za kuwania kiti hiko cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kumalizika kesho tarehe 15 January 2022 saa kumi na nusu.
0 Comments