JIJI LA DODOMA LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA DKT MPANGO LA KUWEKA JIJI SAFI

 


RHODA SIMBA

JIJI la Dodoma limeanza kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango alilolitoa la kuhakikisha jiji  ambalo ni makao makuu ya nchi linakuwa safi na kusisitiza mkataba na Kampuni ya usafi wa mazingira ya Green West iliyokuwa ikihudumu katika jiji hilo.

Agizo hilo limeanza kutekelezwa Jana jijini hapa  chini  ya Mkurugenzi  wa jiji Joseph Mafuru kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo wamekutana na watendaji wa maeneo yote ya jiji la Dodoma na kuweka mikakati ya namna zoezi hilo litakavyotekelezwa .

Mkurugenzi  Mafuru amewataka Watendaji, maafisa afya na Mazingira kufuaata sheria za mazingira kwa kutoa Faini kama kunamtu anastahili adhabu hiyo.

Kuanzia sasa mimi na timu yangu tutanza kutembea mtaa kwa mtaa kata kwa kata ili kuona kama zoezi hili linafanyika ipasavyo kwani niukweli kwamba watu wako makao makuu lakini hawafanyi kazi  kwakazi kunawatumishi wengine wako huko pembezoni wanahitaji kuja makao makuu

Amemuagiza Ofisa utumishi kuorodhesha majina ya watumishi  ambao hawakuweza kufika katika kikao hicho ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru kutowaone muhali watendaji walio chini yake wakiwemo wakuu wa Idara na watendaji wa kata pale anapoona wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwabadilishia vituo vya kazi wale walip chini ya Mamlaka yake.

Pia amesisitiza kuwa uongozi wa jiji hilo kuhakikisha  suala la kuzagaa kwa taka linakuwa historia huku akiweka mikakati kambambe ya kumaliza changamoto hiyo.

Aidha Mtaka amemuagiza Mkurugenzi huyo kuwabadilisha vituo vya kazi watendaji wa Kata na Mitaa ambao utendaji kazi wao umekuwa sio mzuri huku akisisitiza kutoa kipaumbele kwa wale ambao ni watendaji wabunifu.

Hata hivyo kikao hicho cha mikakati ya utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Dkt Mpango kimekuja baada kuwataka viongozi wa jiji la Dodoma  kuhakikisha ndani ya wiki mbili Dodoma ionekane safi katika Kata na Mitaa yote.

Pia ametoa maelekezo  ya kutoonekana kwa kaibada chochote cha machinga katikati ya Mji wala Mitaa kwani machinga wote wameshasajiliwa na kujengewa soko ambapo ameeleza kuwa  kwa kufanya hivyo itasidia kuepusha migogoro  kati ya machinga na Serikali.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Fatma Mganga amewataka Maafisa Mazongira na Maafisa Afya bila kuwasahau Watendaji wote kuwaonyesha wananchi kufanya usafi kwa vitendo na mifano ili iwe njia mojawapo ya kuwaonesha wananchi na wao wahamasike kufanya usafi .

" hapa nimesikia kunajumla ya watendaji 239 walioajiliwa serikalini sasa kunasababu gani ya jiji lionekane chafu...hapa kunamahali hatuwajibiki ipasavyo na iko wazi tumejisahau sehemu  hivyo lazima tujiulize ni kwanini tumefika hapa mpaka viongozi wa juu wanakuja kutukosoa kwamba  sisi Mkoa wa Dodoma  wachafu ," amesema Katibu Tawala huyo. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma  Jabiri Shekimweri amesema mkakati wa usafi wa Mazingira katika jiji la Dodoma liwe la muendelezo ili tuwape imani viongozi wetu wa juu. 

 

 

Post a Comment

0 Comments