📌JOYCE KASIKI
SERIKALI imepanga kupanda miti zaidi ya milioni 14 kupitia wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo vikuu kwa lengo la kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa katika shule ya sekondari ya Dodoma jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Seleman Jafo wakati akizindua kampeni ya upandaji miti kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na Vyuo nchini huku ikiiagiza Maafisa Mazingira nchini kuisimamia miti hiyo kuhakikisha inakuwa kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi.
Wanafunzi waliopo katika shule za msingi na sekondari jumla wapo milioni 14.1 hivyo tumepanga kila mwanafunzi apande mti mmoja ili kufikisha idadi hiyo …,lakini kwa upande wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuna jumla ya wanafunzi 400,000 ambao nao wote watapanda miti.”amesema Jafo na kuongeza kuwa Tunaimani kupitia kampeni hii ya upandani miti kwa wanafunzi wetu kuanzia msingi ,sekondari hadi vyuoni itasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi
Kwa upande wake,Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anaeshughulikia Elimu,David Silinde ameagiza kufufuliwa kwa Klabu za utunzaji wa mazingira katika shule pamoja na Maafisa elimu kuisimamia kwa vitendo kampeni ya soma na mti kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.
Awali,mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Dodoma Monica Marwa ametoa rai kwa jamii ya watanzania kupanda miti na kuitunza kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa huku akiiomba Serikali kuwachimbia kisima ili waweze kumwagilia miti ambayo itapandwa nchini kote.
0 Comments