DKT.TULIA:HAKUNA SHERIA INAYONIZUIA KUGOMBEA USPIKA

 

 

 

DKT. Tulia Ackson ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa Bunge

 Dkt. Tulia amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni Bw. Solomon Itunda katika Ofisi za Makao makuu ya CCM Dodoma,naibu spika amesema hakuna sheria yeyote ya Bunge inayomzuia yeye kufanya hivyo.

Dkt.Tulia amesema Katiba imewataja Waziri na Naibu Waziri kama kundi ambalo halitakiwi kugombea nafasi hiyo na haijamtaja Naibu Spika.

Kwa mujibu wa katiba hakuna sheria yoyote ya Bunge inayomzuia Naibu Spika kugombea nafasi ya U-Spika, sio kwasababu nimechukua fomu basi nafasi ya U-Naibu spika iko wazi hapana

Dkt. Tulia Ackson


 


Post a Comment

0 Comments