DKT.MPANGO ATOA SIKU 7 JESHI LA POLISI KUPELEEKA TAARIFA MAUAJI YA WATU 5 WA FAMILIA MOJA DODOMA

 



📌RHODA SIMBA NA JOYCE KASIKI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Philip Mpango ametoa siku 7 kwa jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linawasilisha  taarifa rasmi kwenye ofisi ya Rais juu ya mauaji ya watu watano wa familia moja yaliyotokea katika kijiji cha Zanka kilichopo  Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.

Kadhalika amelitaka jeshi hilo kufanya kazi usiku na mchana kuwasaka wahalifu waliofanya  mauaji  hayo ambapo baba, mama, watoto wawili na mjukuu walishambuliwa hadi kifo na watu wasiojulikana.

Pia Dkt.Mpango amewasihi wananchi kujenga mahusiano ya kuwa wanajuliana hali kila siku na kila wakati ili kugundua mapema matukio kama hayo.

Dkt Mpango ameyasema hayo leo Januari 26 jijini hapa alipofika katika  kijiji hicho  kwa ajili ya kutoa pole kwa familia iliyo ondokewa na wapendwa wao waliouwawa  wiki iyopita ambapo waligundulika baada ya siku tatu mara tukio hilo la mauaji lilipofanyika.

Tukio hili ni la kinyama,haliwezi kuvumilika naagiza Jeshi la polisi ndani ya siku saba tupate majibu ya watu hawa waliofanya tukio hili la kinyama namna hii,majirani ndugu pia lazima wahusike kuisadia Jamhuri haiwezekani watu waishi bila kutembeleana wala kujulina ha hali

Aidha amesema nchi  imekuwa ya amani siku zote Serikali haiwezi kukubali kuongoza  nchi katika hali hiyo na kwamba jeshi la polisi lifanye uchunguzi haraka watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Hivyo,Dkt. Mpango amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP )Simon Sirro kuhakikisha mauaji yanakoma nchi nzima na kuhakikisha wahalifu wa mauaji hayo wanapatikana ndani ya siku saba

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma ,nifikishie salam kwa IGP ,mauaji haya nchi nzima yakome,mfanye kazi ya kuyazuia,Polisi mna kazi kubwa ya kufanya nchi nzima

Dkt. Mpango pia ameshangazwa kutokea kwa mauaji hayo na marehemu kukaa siku tatu na kuharibia ndani bila majirani wala uongozi wa kijiji kutokuwa na taarifa 

SOMA HII PIA 👉👉DARAJA LA TANZANITE KUANZA KUTUMIKA FEBRUARI MOSI

Hivyo amewataka wananchi  kujenge tabia ya kupendana, kujuliana hali na  pale ambapo kuna matatizo kwenye jamii  hata ya  kimila wakae kuyazungumza kuliko kuwa na visasi  ambavyo havina tija.

 Niwaombe kwanza familia zetu zote katika kata hii ya Zanka na nchini kote ,watanzania duniani tunasifika kwa upendo inakuwaje mwanafamilia haonekani siku tatu na wanafamilia wapo karibu ,hata hodi nyumba hii hakuna?

Pia Dkt.Mpango amewataka  viongozi kuanzia ngazi ya ubalozi kufuatilia maisha ya wananchi huku akiwaasa viongozi wa dini kwenye nyumba za ibada  kuwakumbusha wananchi kwamba hakuna binadamu mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu mwingine .

UMEISOMA NA HII? 👉MRADI WA AKILI BANDIA WAZINDULIWA UDOM,TANZANIAKUTENGENEZA ROBOTI 2024


 

Post a Comment

0 Comments