DKT GWAJIMA AFURAHI 'MACHINGA' KUWEKWA KUNDI MAALUM

 


📌MJJWM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaheshimisha sana kama Wizara, mara baada ya kulitambua kundi la Machinaga kama kundi maalum, na kuliweka chini ya Wizara hiyo ili kero zao ziweze kutaliwa kwa haraka na kwa wakati.

Waziri Dkt. Gwajima, aliyasema hayo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuia ya Wamachinga nchini Mapema juma hili Ofisini kwake kwenye Mji wa Serikali Mtumba, ambapo alisema niwakati muafaka kwa Jumuiya hiyo kuwa karibu na seriakli kama serikali ilivyo watambua.

Tunatambua na kuthamini mchango wenu, maana katika jamii zetu hakuna ambaye hajawahi kunufaika na bidhaa za machinga mmekuwa mikitusogezea bidhaa kwa ukaribu zaidi, hivyo ni jukumu la Wizara ninayo isimamia kuhakikisha tunaweka mazingira salama na rafiki kwa makundi yote ikiwepo kundi la Machinga kwa ustawi wa Taifa letu

Waziri Gwajima

Waziri Dkt. Gwajima amema, ili kujenga umoja wa maono kwakwenda mbele zaidi, ndio sababu yakuwaita na kuomba kuzungumza na viongozi hao ikiwa ni mwanzo wa kwenda kwenye makundi yote na kufahamu fursa walizo nazo na kuzifanyia kazi.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Ernest Matondo, alisema kutambuliwa kwa kundi la Machinga na kuwekwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, imekuwa ni hatua kubwa, kwani katika kipindi cha nyuma walikuwa hawajui, kundi hilo linaangukia sehemu gani.

Hatua hii ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, sisi tunaipongeza sana, maana kuanzia mwaka jana 2021, serikali yetu imekuwa mstari wa mbele kupigania haki zetu, ikiwepo kikao chetu na Waziri Mkuu ambacho tunaimani ndio matokeo tunayo yaona  sasa hata kuweka chini ya Wizara na changamoto zetu kutafutiwa ufumbuzi
Matondo.

Mwenyekiti huyo, alisema kwa sasa tayari Jumuiya ya Machinga nchini imefanya mazungumzo na baadhi ya Benki za Kibiashara na kukubaliana kwa namna gani wataweza kuwakopesha mitaji kwa kutumia dhamana ya vizimba vyao, Pamoja nayo Mwenyekiti huyo amesema pia hivi sasa wamefanikiwa kuwapanga wamachinga katika miji ya Mbeya, Mwanza nah atua waliyonayo nikwenda Mtwara kuwapanga wamachinga wa huko.

Awali akimkaribisha Waziri mwenye dhamana kwa ajili ya kuzungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na makundi Maalum, Amon Mpanju, amesema wito wa viongozi hao unafatia kundi hilo kujumiishwa katika wizara husika  hivyo ili kutambua ni mambo gani wanataka wizara ifanye kwa upande mmoja nawenyewe watakuwa na jukumu lipi ndio sababu yakufanya mazungumzo na viongozi hao wa jumuia ikiwa ni hatua za awali katika kudumisha ustawi wao.

 

Post a Comment

0 Comments