BASHE:HAKUNA MTANZANIA ATAKAYEKUFA KWA NJAA

 


📌JOYCE KASIKI

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema hakuna Mtanzania yoyote atakayekufa na baa la njaa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha kutokuwepo kwa mvua kwani serikali ina akiba ya kutosha ya chakula.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Waziri Bashe wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Watanzania hamna sababu ya kuogopa mabadiliko ya hali ya hewa yanayochangia kutokuwepo kwa mvua…,Serikali yenu ipo pamoja na ninyi kuhakikisha hampati tatizp la upungufu wa chakula.

Bashea kuongeza kuwa

 “Hakuna mtu atakayekufa na njaa Serikali inaakiba ya chakula cha
kutosha hivyo hakuna sababu ya kuhangaika,”
kwa mujibu wa Waziri huyo chakula kipo cha  kutosha katika maghala hivyo hakuna haja ya kuingia woga wowote kwani  serikli haitaruhusu wafanyabiashara wauze mazao kwa bei ya juu.

Amesema kuna mifumo mingi ambayo itatumika kuhakikisha wananchi wote wanapata chakula cha kutosha .
Kutokana na hilo amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wowote juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA yanayosababisha mabadiliko ya mvua.
Amezungumzia kuhusu kupanda kwa bei yam bole hapa nchini huku akisema bidhaa hiyo imepanda karibu duniani kote.

 Bei ya mbolea imepanda duniani kote hivyo kila mmoja anapaswa kulijua hilo lakini serikali ipo pamoja kuhakikisha suala hilo haliwaletei shida wakulima

amesema Bashe.

Akizungumzia kuhusiana na mazao ya kahawa,ndizi na mengineyo amesema serikali inakwenda kubadilisha mifumo ili kuhakikisha wakulima hawachajiwi fedha kubwa na badala yake itashushwa ili iwe sawa kwa wakulima wote.

Amesema wakulima wanapaswa kuwa wavumilivu kutokana na serikali kuwa pamoja na wao katika suala zima la kilimo kwa jamii nzima inayowazunguka.

Amesema lengo la serikali ni kuona kilimo hapa nchini kinasonga mbele na si kurudi nyuma ili watu waweze kujikimu kupitia Kilimo

Post a Comment

0 Comments