📌RHODA SIMBA
MSAJILI wa Baraza la
Famasia nchini Elizabeth
Aidha amesema pia kutotumia dawa
kwa usahihi pia kunaweza kusababisha vifo, maradhi ya figo na ini na usugu wa
vimelea katika ugonjwa.
Ameyasema hayo leo
Disemba 10 jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa
habari ambapo amesema kumekuwa na mazoea ,ya
wananchi kujichukulia dawa bila usahihi pasipo kufuata ushauri wa
wataalamu wa afya.
“Ni vyema wananchi mkafahamu kuwa
zipo athali za matumizi yasiyo sahihi ya dawa ikiwemokuongezeka kwa ugonjwa,
kutopata nafuu,kutopona na hatimaye kupelea kifo,matumizi ambayo huongeza
gharama za matibabu,kuongezeka kwa madhara na usugu wa vimelea vya
magonjwa katika dawa na kusababisha maradhi ya figo na ini,”amesema
Amesema zipo faida zitokanazo na
matumizi sahihi ya dawa ikiwemo kupunguza uwezekano wa kujenga usugu wa
vimelea , kupunguza maradhi yatokanayo na usugu wa vimelea vya magonjwa.
Ametaja faida nyingine kuwa ni
kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na utumiaji
usugu wa dawa , kuboresha af ya mtumiaji wa dawa hivyo kupona kwa
wakati pamoja na kjenga imani na mifumo ya kutolea huduma za afya.
Katika hatua nyingine
msajili huyo amewataka wafamasia wote nchini kuakikisha wanauhishwa leseni zao
kabla ya 30 Disemba mwaka huu kupitia mfumo wa kielekroniki
ili ili kurahisha utendaji.
Kuhusu udhibiti wa maduka ya
famasi Msajili huyo amesema mkakati ikiwemo kuendelea na ukaguzi wa kila siku
wa kukagua ili kubaini wanaokiuka na sheria kuchukua mkondo wake.
Natoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata dawa katika maeneo ambayo yamesajiliwa na kwa duka la dawa ambalo litatoadawa bila cheti cha daktari adhabu yake ni faini isiyopungua milioni tano au kifungo cha miezi 12
Shekalaghe amewataka wamiliki wa famasi wanaoongeza marembo au kuweka matangazo ili kuvutia wateja kuacha mara moja kwani ni kinyume na kanuni za afya
“Niwaombe sana wamiliki wa maduka
ya famasi kuacha mara moja na endapo tutakuta kuna ukiukaji wa sheria au kanuni
tumeelekezwa kufunga famasi hiyo,”amesema
0 Comments