📌RHODA SIMBA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema jumla ya silaha 228, zimesalimishwa kwa Jeshi la Polisi huku silaha aina ya gobore imeoneka ikiongoza kwa asilimia 76.3.
Kadhalika ameliagiza jeshi hilo kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015.
Ameyasema hayo leo December 6 jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari , kuhusu utekelezaji wa tangazo la msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu lililoanza mnamo Novemba 1 hadi 30 mwaka 2021
Amesema kufanya hivyo ni kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobore kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi katika jamii.
Kwa mchanganuo wa PISTOL 05 sawa na 2.2% ya silaha zote zilizosamilishwa, magobore 174 sawa na 76.3% ya silaha zote zilizosalimishwa, S/gun 38 sawa na 16.7% ya silaha zote zilizosalimishwa, Rifle 10 sawa na 4.4% ya silaha zilizosalimishwa na SMG 01 sawa na 0.4% ya silaha zote zilizosalimishwa
Pia imesalimishwa jumla ya mitutu 12 ambapo mitutu 11 imesalimishwa Mkoa wa Tanga na Mtutu 01 umesalimishwa Mkoa wa Mbeya.
Amesema kufuatia matokeo haya ya usalimishaji wa silaha haramu,Waziri Simbachawene amelielekeza Jeshi la Polisi kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za Ulinzi katika jamii.
Pia,kufanya misako kwa
kutumia taarifa za kiintelelijensia ili kuwabaini
na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria na
kisha kuwachukulia hatua za kisheria.
0 Comments