📌MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirisha jumla ya kontena 93 ya gundi ( utomvu) ambayo sawa na tani 1683 iliyokuwa tayari imeshavunwa wakati akitoa tamko la kuzuia usafirishaji wa malighafi hiyo kwenda nchi za nje
Ametoa
kauli hiyo leo Jijini Arusha mara baada ya kupokea ushauri kutoka
kwa Kamati ya Kumshauri Waziri kuhusu masuala ya misitu kabla ya
kufanya mkutano wa Wadau wa mazao ya misitu kuwa gundi hiyo ambayo
imekwisha vunwa inapozidi kukaa inapoteza ubora wake na hivyo kutokufaa
tena kwa matumizi tena
Dkt.Ndumbaro
amesema amelazimika kuruhusu kusafirishwa kwa tani hizo ili gundi hiyo
isiweze kuharibika pamoja na kuepusha hasara ambayo ingewapata kwa
wamiliki pamoja na serikali kukosa mapato kwani Serikali inapata mapato
pindi malighafi hiyo inaposafirishwa.
"
Hii gundi ni 'Chemicals' inavyozidi kukaa inabadilika rangi na
Wataalamu wamenambia kuwa ikiendelea tu kukaa muda wake unaisha wa
matumizi " amesisitiza Dkt.Ndumbaro.
Gundi
ni aina ya utomvu unaogemwa kwenye miti ya kupandwa aina ya misindano
ambapo malighafi hiyo husafirishwa kwenda nchi za nje lakini hata
hivyo hadi hivi sasa matumizi yake bado hayajaweza kufahamika kuwa
inatumikwa kwa ajili ya kutengenezea vitu gani
Hatua
hiyo inakuja kufuatia agizo la kusitishwa kuvunwa na kusafirishwa kwa
malighafi hiyo kwenda nchi za nje alilolitoa Dkt. Ndumbaro mwezi
Oktoba akiwa mkoani Iringa mara baada ya kushindwa kupata maelezo ya
kutosha kuhusiana na biashra ya bei ya gundi hiyo pamoja na matumizi
yake huko inakosafirishwa nchi za nje hususani China
Katika
hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameendelea kushikilia msimamo wake wa
kusitisha zoezi la kuvuna utomvu huo hadi pale Chuo cha Kilimo cha
Sokoine ( SUA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania ( TAFORI)
zitakapotoa utafiti wake ambao kwa sasa bado haujakamilika juu ya
athari ya miti inayovunwa gundi hiyo
Akifafanua
katazo hilo Dkt.Ndumbaro amesema katazo hilo lina manufaa makubwa kwa
Watanzania kwa ajili ya kutengeza ajira nyingi kwa wananchi
''Mara
baada ya kukamilika kwa ripoti kutoka TAFORI na SUA na kujiridhisha
kuwa uvunaji hauna madhara wafanyabiashara mtatakiwa kujenga viwanda
hapa nchini na sio habari ya kusafirisha'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Akizungumzia
kuhusiana na Biashara ya Veneer, Dkt. Ndumbaro amewaeleza
Wafanyabiashara hao kuwa yeyote atakayetaka kusafirisha lazima afuate
masharti aliyoyato mwezi Noemba akiwa Jijini Dar es Salaam huku akiwata
raia wa China wanaofanya biashara hiyo kupitia Chama cha Wafanyabiashara
wa China kilichopo nchini kama Wadhamini
0 Comments