📌RHODA SIMBA
REDIO za kijamii
zimetakiwa kuendelea kuandaa maudhui yanayozingatia maadili na miiko ya
kitanzania.
Kauli hiyo imetolewa
leo Disemba 7 jijini hapa na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Emmanuel Buhohela wakati akifungua
kongamano la redio za kijamii lililoandaliwa na mtandao wa
redio za kijamii Tanzania ( TADIO) ,Mtandao wa Kutoa Huduma za
Redio Afrika Mashariki (EARS) na Shirika la Habari la Kuchochea
Mabadiliko la Ujerumani.
Amesema Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini umuhimu
wa vyombo vya habari hasa redio za kijamii ambazo
zinawafikia watu wengi hasa sehemu za vijijini .
Aidha amezitaka redio
za kijamii kuendelea kuandaa maudhui yanayozingatia maadili na miiko ya
kitanzania.
Amesema mchango
wa redio za kijamii ni mkubwa kwani wananchi wengi wanafikiwa na redio hizo
zimekua ni sehemu muhimu za kusambaza taarifa na ni ukweli ulio
wazi kwamba uandishi wa habari zinazojali
maisha na kero za watu huchangia kwa kiasi kikubwa kujenga uelewa na
kupunguza umasikini .
TADIO mnafanya kazi kubwa sana, nimeambiwa mtandao wenu unawafikia asilimia 70 ya Watanzania hasa waliopo vijijini. haya ni mawanda makubwa sana ya kuifikia jamii kimawasiliano
Amesema Serikali inafanya kila juhudi kuimarisha umoja wa wana Afrika ya Mashariki na uimara wa Jumuiya ya watu wa Afrika Mashariki inategemea ubadilishanaji wa taarifa,uwepo wa redio hizi za kijamii na mahusiano yatakayo imarisha umoja huo na kubadilisha taarifa , ujuzi wa kitaalamu na hata fursa ambazo zinaweza kuchangia maendeleo .
Amesema kuna
changamoto nyingi zinazozikabili radio za kijamii ikiwemo uwezo
mdogo wa kifedha , uwezo wa kitaaluma miongoni mwa watendaji
changamoto ya tozo na kodi mbalimbali.
“Niwahakishe kwamba serikali inajitahidi sana kuhakikisha kwamba tasnia ya habari inakuwa hasa maendeleo endelevu ya redio za kijamii . kwa hili naomba tukae pamoja , tutafakari na tupange mipango ya pamoja ya kuwa na mipango endelevu ya kuziimarisha redio zetu na kuondoa vikwazo,” amesema Buhohela
Nae Kaimu mkurugenzi
wa TADIO, Baptist John amesema TADIO ina wanachama 34 na press club moja
ambayo ni ya Pemba.
Hata hivyo amesema
uanzishwaji wa redio jamii sio rahisi na changamoto iliyopo ni uendeshaji na
namna ya kuwawezesha waandishi kuwa na mapato yanayojitosheleza ili kuwasaidia
wasiwe wanapotosha taarifa katika jamii.
0 Comments