📌MWANDISHI WETU
TAASISI ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) mwishoni mwa wiki imewajengea uwezo
waandishi wa habari mkoa wa Dodoma kuhusu sheria mbalimbali za habari .
ikiwemo kujadili faida na changamoto za baadhi ya vifungu vya sheria hizo
katika tasnia ya habari nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa MISA
TAN,afisa Habari wa taasisi hiyo Jackline Jones ambaye pia ni mratibu wa mradi
huo wa kuwajengea uwezo unaofadhiliwa na taasisi ya International Media Support(IMS)
amesema lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi hao ili kutambua
maudhui ya sheria hizo.
“Tunachojaribu kupitia semina ni kuwaonesha na
kuwasaidia Waandishi wapate Uelewa wa sheria ambazo zinasimamia tasnia
yao.”Amebainisha Jackline
Afisa huyo amesema kupitia semina hiyo waandishi
watakuwa na uwezo wa kushiriki mijadala mbalimbali ikiwemo ile ya mabadiliko ya
baadhi yaa vifungu katika sheria hizo ambazo zinaonekana kuminya uhuru wa
kujieleza.
Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo Jesse Mwandishi
na Mhariri Mwandamizi Jesse Kwayu
amebainisha kwamba yapo mambo mengi mazuri kwenye sheria za habari lakini mazuri hayo yanafunikwa na vifungu
vichache vinavyominya uhuru wa habari na kujieleza.
Kwayu pia amewataka waandishi wa habari kuzisoma
sheria hizo na kuzielewa ili wawe na uelewa juu ya vifungu mbalimbali katika
sheria hizo.
"Sheria tulizonazo ukizisoma kwa wepesi
utaziona ni nyepesi lakini ni sheria nzito sana,na Mwandishi ili akamilike
lazima azifahamu sheria hizi"-amesema Kwayu
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Kiraia mkoa
wa Dodoma Menas Muhumpa amewataka waandishi wa Habari kushirikisha taasisi hizo
katika mapambano ya kudai haki kujieleza kwa vile ni matakwa ya katiba.
Muhumpa amesema haki hiyo inamgusa kila mwananchi hivyo ni vyema taasisi zote
zikaungana kupigania haki hiyo.
“Msione hili jambo ni kwenu peke yenu,kama hivi MISA
TAN walivyotushirikisha basi iwe fursa kwa taasisi nyingine za habari kuona
umuhimu wa kushirikisha taasisi za kiraia ili kuunganisha nguvu na kuwa sauti
ya pamoja.” Amebainisha Muhumpa.
Kwa upande wa Wandishi washiriki wa mafunzo
hayo,wamewataka waandishi kuungana pamoja katika kutetea maslahi ya tasnia.
Merciful Munuo ni mmoja wa Wanahabari walioshiriki semina hiyo amesema kuna
mambo mengi yanayosonga utendaji wa wanahabari nchini lakini kwa mara kadhaa
waandishi hawatoi ushirikino katikakutatua changamoto za wengine.
“ Tuungane pamoja katika harakati za kudai uhuru wa habari,linapomtokea
mwenzako leo kesho linaweza kuwa kwako.Mmoja wetu akipatwa na tatizo tusimuache
yeye na chombo chake tu.” Ameelezea Munuo.
0 Comments