📌RHODA
SIMBA
NAIBU
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu) Gerald
Mweli amezitaka Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu kutoa mafunzo kwa walimu
wapya ili kuwajengea uwezo kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Pia
ameziagiza kamati hizo kutoa mafunzo kwa walimu ambao wanaonekana kukiuka
maadili ya taaluma hiyo na kufanya makosa ya mara kwa mara ili warudi kwenye
mstari na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza na Kamati hizo kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Magharibi Mweri amesema,mafunzo hayo yatasaidia makundi hayo kufanya kazi yao kwa kufuata miongozo,sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya kada hiyo ya ualimu.
Mafunzo haya mnayoyapata na ninyi mkayatoe kwa walimu wapya huko katika maeneo yenu ,lakini pia wapo walimu ambao walishapewa mafunzo lakini bado wamekuwa wakifanya makosa ya kujirudia rudia,nao nendeni mkawaite na kuwapa mafunzo badala ya kukimbilia kuwapa adhabu
Aidha
alisema kamati hizo zimepewa jukumu la kufuatilia maadili ya walimu huku
akisema wanapaswa kuliangalia suala hilo kwa umakini mkubwa na kutoa adhabu
inayomstahili mwalimu kulingana na kosa alilolitenda.
“Mkumbuke
mmepewa jukumu na mustakabali wa ajira za walimu upo mikononi mwenu,maamuzi
mnayoyafanya ni ya kutazamwa na kuyafanya kwa kutenda haki ,kwenye kosa mwalimu
apewe adhabu anayostahili lakini msisubiri watu wafanye makosa ili wawaadhibu,
“Muwajengee
walimu wapya uwezo ,pia na walimu ambao hawaendi sawasawa muwape mafunzo ,maana
Serikali haipendi mwalimu afukuzwe kazi maana unakuta wengine tayari wana
uzoefu wa miaka kumi,kwa hiyo tunapenda wabaki shuleni .”amesema Mweri
Mweri
amezitaka kamati hizo kuhakikisha chombo hicho kinakuwa baraka katika kutatua
na kupunguza changamoto za walimu badala ya chombo hicho kugeuka
laana .
Amesema,kwa
upande wa Tamisemi ,itaendelea kushirikiana na TSC katika kuhakikisha mnapata
vitendea kazi .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Profesa Willy Komba amesema mafunzo hayo yatawawezesha watendaji hao kusimamia sheria kanuni na taratibu kama zilivyowekwa katika ajira zao.
“Tume
hii imeamua kuendelea kuwapatia watendaji mafunzo ili wajitambue wao ni wakina
nani na si kuwaacha wafanye makosa ndipo waadhibiwe au kufukuzwa
kazi,ukishamfukuza mwalimu kutafuta pengo lingine la kuziba ni kazi, hivyo
tutaendelea kutoa mafunzo haya kwa awamu kutokana na upatikanaji wa fedha”
amesema Profesa Komba
Aidha amesema,tangu waanze kuwawezesha watendaji hao wa kamati za wilaya malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa na tayari wameshazifikia kanda tano kwaajili ya utoaji mafunzo hayo.
Awali,Katibu Tume
ya Utumishi wa Walimu nchini (TSC) Paulina Nkwama amewataka
wajumbe wa kamati hizo za wilaya kuwa wasikivu kwa kuwa watajifunza
mafunzo ambayo yatasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
0 Comments