📌 MWANDISHI WETU
MWANDISHI Mkongwe na Mchambuzi wa siasa Jenerali Ulimwengu
amewataka wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini kushirikiana na waandishi wao
katika mapambano dhidi ya Uhuru wa Habari.
Ulimwengu amesema wamiliki wa vyombo vya habari
wanatakiwa kujua kwamba licha ya kuwa wamiliki wa vyombo hivyo lakini lengo kuu
ni kuhudumia jamii .
Akizungumza jijini Dodoma katika mjadala wa wamiliki wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN),Ulimwengu amewataka wamiliki hao kutokuwa sehemu ya ukandamizaji wa Uhuru wa habari kwa maslahi yao binafsi.
Kuna watu wanaanzisha vyombo vya habari lakini lengo ni kulinda itikadi zao za kisiasa maslahi ya biashara zao au marafiki zao wanasahau kwamba vyombo wanavyoanzisha ni mali ya wananchi,kwa sababu vyombo vyote vinaanzishwa ili kuhudumia wanannchi
Jenerali amesema kwa kipindi cha miaka kadhaa nyuma
tasnia ya habari imekuwa mfu kutokana na sababu mbalimbali lakini amesema
wamiliki wa vyombo vya habari hawawezi kukwepa kudorora huko kwa tasnia muhimu
katika jamii.
Ulimwengu amewataka wamiliki ambao kama wanaona
hawapo tayari kufanya na kuhudimia jamii ni bora wahamishie mitaji yao katika
shuguli nyingine ili kuacha nafasi hiyo kwa watu wenye nia ya dhati ya kusaidia
kupaza sauti za wananchi ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Kama una chombo cha habari na hakiwajibiki kwa wananchi ni bora ukafanye kazi nyingine,kazi ya habari inabidi ujikane hadi nafsi yako na kuwa ‘commited’ kwenye kufanya kazi hiyo
Hata hivyo Ulimwengu amewashauri wamiliki hao kuweka
utaratibu mzuri utakaowawezesha waandishi wao kujiendeleza kielimu ili kuongeza
maarifa yatakayowasaidia kuchakata kwa weledi maudhui wanayoyapeleka kwa
hadhira yao.
Kwa upande wake Mhariri Mwandamizi mstaafu Jesse
Kwayu amewataka wamiliki kushirikiana na watendaji wao (waandishi) ili kuweza
kurudisha heshima ya vyombo vya habari nchini kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
“Vyombo vya Habari kwa sasa haviogopwi kama
zamani,Wamiliki ni lazima kushiriki katika harakati za kurudisha vyombo vya
habari kurudisha ‘lost glory’ (heshima iliyopotea) katika tasnia ya habari”
amesema Kwayu.
Kwa upande wao wamiliki wa vyombo vya habari wameibua changamoto mbalimbali
ambazo zikirekebishwa zinaweza kurudisha heshima katika tasnia ya habari
Mmiliki wa Standard FM (Singida) Daudi James amesema tabia ya waandishi wa habari
kuendekeza ‘bahasha ya kaki’ (posho) imekuwa tatizo kubwa katika kutengeneza
maudhui yasiyo na faida kwa jamii zaidi ya kumtangaza yule aliyewalipa posho.
Bahasha(posho) zinatuulia vyombo vya habari,waandishi wengi hawaandiki habari za uchunguzi wanakimbilia kwenye habari zenye posho tu.
Kwa upande Abdul Diallo akimuwakilisha mmiliki wa
kampuni ya Sahara Media Group amesema baadhi ya Wahariri na Waandishi
wanashiriki kuminya uhuru wa habari kutokana na kuendekeza itikadi zao za
kisiasa.
Dialo amesema katika kipindi cha uchaguzi mkuu
uliopita wapo baadhi ya Wahariri na waandishi waandamizi waligombea nafasi mbalimbali
katika vyama vya siasa,amesema tukio hilo lilidhhirisha kwa namna gani
waandishi wenyewe wana pande ambazo wanazitumikia.
“Kuna
wamiliki ni wanasiasa lakini hawaingilii vyombo wanavyovimiliki lakini kuna
baadhi ya matukio ya uminywaji wa uhuru wa kujieleza tatizo ni itikadi za
wahariri wa habari wamiliki hawatakiwi kulaumiwa”alifafanua Dialo.
Mjadala huo
umefanyika wiki hii ukiwa na lengo la kuwajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya
habari kuhusu kazi ya vyombo vya habari kwenye kuchochea uwazi, haki na
demokrasia.
Lengo jingine la mjadala huo kutafuta ufumbuzi
wa changamoto zinazoathiri uhuru wa kiuhariri unaosababisha kutokuwepo kwa
uhuru wa kiuhariri kwenye vyombo vya habari unapelekea vyombo vya habari
kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii.
0 Comments