📌RHODA SIMBA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewaagiza Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Watendaji wa Halmashauri zote nchini kusimamia kusiwe na vikwazo kwa wanafunzi pale wanapoenda kujiunga na kidato cha kwanza.
Kadhalika amewataka wakuu wa shule kuzingatia kwamba kuna baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika familia duni na pale wanapoenda kujiunga na shule wasiweke masharti magumu hususani kwenye mahitaji ya kwenda nayo shule ambayo yatawafanya washindwe kujiunga.
Ameyasema hayo leo octoba 24 jijini hapa wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 ambapo jumla ya wanafunzi 907,802 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.
“Tarehe 30 Octoba Baraza la Taifa la mitihani lilitoa matokeo ya waliomaliza darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi waliofanya mitihani milioni moja 107,460 na kwamba kati ya hao wanafunzi laki 907,802 wamefaulu katika mitihani hiyo,
“Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya elimu imekamilisha zoezi hilo la kuwapangia wanafunzi shule kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na zoezi hili limehusisha jumla ya wanafunzi 907,802 kati ya hao wasichana 467,967 wavulana 439,835 sawa na asimilia 81.9 ya wanafunzi waliyofanya mitihani ya kuhitimu” amesema Ummy
Aidha amesema kati ya wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu waliofanikiwa kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 2673 ni wanafunzi wenye mahitaji maalumu sawa na asilimia 0.29 ya wanafunzi wenye ulemavu ambapo kati ya hao wavulana ni 1471 wasichana 1202.
Tumeangalia wanafunzi waliofaulu mwaka jana kulinganisha na mwaka huu ambapo tumeona kumekuwa na ongezo la wanafunzi 73,932 sawa na ongezeko la asilimia 8.87
Akizungumzia kuhusu mfumo wa uchaguzi amesema mwaka huu uchaguzi wa wanafunzi umefanyika katika mfumo wa kielectronic ambapo umesaidia mambo kadhaa ikiwemo kupunguza muda wa uchaguzi, gharama, na upangaji wa wanafunzi na limeondoa upendelo na mfumo umetenda haki kwa kuangalia ufaulu wa juu.
“Nipende kusema kuwa mfumo umeongeza ufanisi kutokana na wanafunzi kupangwa kama mfumo unavyoelekeza na Serikali imefanya maandalizi mapema ya wanafunzi wote wamechaguliwa kujiunga na shule zetu za sekondari na wataanza siku moja mara muhula utakapoanza na tunatarajia utaanza tarehe 17 january “
Matarajio yetu kwa jitihada za serikali wanafunzi wote watakuwa darasani kwa siku moja na nichukue nafasi hii kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha shilingi billion 240 katika ujenzi wa madarasa elfu 12 nchi nzima
Hata hivyo mesema Vigezo
vilivyotumiwa kwa wanafunzi katika ufaulu ni kupata asilimia 121 hadi 300 kwa
alama 300 ambapo kila somo lilikuwa linabeba alama 50 katika kila somo
kwa masomo sita.
0 Comments