📌RHODA SIMBA, DODOMA.
NI Majumaa kadhaa yamepita tangu wekundu wa msimbazi Simba
waachane na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Didier Gomez da
Rosa ambae alihudumu kwa msimu mmoja tu.
Mara baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa na nafasi yake kukaimiwa na kocha msaidizi Thiery Hitimana kwa kushirikiana na Suleiman Matola mpaka pale Simba walipomtangaza Pablo Franco Martini kama kocha mkuu.
Mara baada ya Simba kumtangaza Pablo kuwa kocha mkuu wa Klabu hiyo kumekuwa na maneno yanayosemwa kuhusiana na maisha yake ya soka hususani timu ambazo amewahi kuzifundisha ikiwemo Real Madrid ambapo alikuwa kocha msaidizi chini ya mfaransa Zinadine Zidane mwaka 2018/2019.
Kuna picha inayo onesha kuwa ni ukurusa rasmi wa Twitter ya
Real madrid C.F. ikionesha timu ya hiyo imempongeza Pablo Franco MartÃn
kwa kujiunga na Simba katika tasfri isiyo rasmi ya kiswahili
inasema “Klabu inatoa shukrani zake za dhati kwa kocha wetu msaidizi @
pablofrancomartin kwa kufanya kazi nasi kama kocha msaidizi.Tunatakutakia
mafanikio mema kwenye Klabu yake mpya ya Simba Asante Pablo
Ukweli ukoje
Ukweli ni kwamba habari
hiyo siyo ya kweli.Kwanza ukurasa uliotoa habari hiyo siyo ukurasa
rasmi wa twitter wa timu ya Real Madrid bali ni moja kati ya
ukurasa za mitandaoni zinazotumika kutoa taarifa za uzushi.
Central Press Club imefanya tafiti kwenye kurasa rasmi zote
tatu Twitter ya Real Madrid @realmadrid ambazo zipo katika lugha ya
kiingereza, kifaransa na kihispaniola na kugundua kuwa hakuna salamu za namna
hiyo na ni uzushi mtupu unao sambazwa.
Jambo lingine linalotia
shaka katika Twitter hiyo ya uongo ya real madrid ambayo imenukuu Twitter
ya uongo ya kocha mpya wa Simba kwa kuandika@ pablofrancomartin wakati
ukweli ukurasa rasmi wa kocha huyo mpya wa simba Pablo Franco MartÃn ni@FrancoMPablo.
Pia kurusa zote zilizothibitishwa na Twitter
ziwe za taasisi ama mtu mmoja mmoja zimekuwa na alama au tiki ya blu lakini hii
inayodai ni ukurasa rasmi wa Klabu ya Real Madrid na ambayo inadai
umethibitishwa imewekewa alama au tiki nyeupe badala ya blu.
Licha ya Pablo Franko Martini kuwahi kufundisha
timu mbalimbali ikiwemo Real Madrid kama kocha msaidizi, Beijing kama
kocha msaidizi ,,Getafe CF kocha mkuu, CD PUERTOLANO kama
kocha mkuu, pamoja na CD SANTA EUGENIA kama kocha mkuu lakini Real
Madrid hawajampongeza ni uzushi mtupu.
0 Comments