📌RHODA SIMBA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthon Mtaka amesema Serikali inatambua umuhimu wa vyuo vya ufundi na amewataka vijana wenye fani ya ufundi ujenzi kuchangamkia fursa ya kujenga vyumba vya madarasa jijini hapa vyenye thamani ya shilingi bilioni 14 .
Aidha fedha hizo ni zile zilizotolewa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoka benki ya dunia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mpango wa maendeleo ya ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.
Ameyasema hayo jijini hapa katika mahafali ya 36 ya chuo cha ufundi stadi Don bosco kilichopo nje kidogo ya jiji la Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine Mtaka amewatunuku vyeti wahitimu 150 katika ngazi ya cheti na stashahada katika fani mbalimbali.
Mtaka amesema kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa vijana wenye ujuzi mbalimbali ikiwemo ufundi ili waweze kunufaika na fedha hizo kama Serikali inavyoelekeza hivyo na kuwataka uongozi wa chuo hicho kuwasilisha majina ya wahitimu ofsini kwake ili waweze kutafutiwa fursa hizo.
"Mpango wa Serikali ni kuhakikisha inajali vijana na hii nchi ina changamoto ya mafundi japo ajira zipo, lakini tatizo linakuja kwa vijana wenyewe wanapopelekwa kwenye soko la ajira wanaanza kuiba vifaa,na kuonesha tabia zisizofaa mpaka kupelekea kufukuzwa sasa hivi tunajenga vyumba vya madarasa hapa Dodoma vyenye thamani ya shilingi bilioni 14 niwatake mkachangamkie fursa."amesema Mtaka
Katika hatua nyingine ameutaka uongozi wa chuo hicho kuwa wabunifu ,kuwa na ushindani katika soko la ajira ambapo amewataka kuanzisha kampuni tanzu ya kufanya shughuli mbakimbali kutokana na fani walizonazo ili chuo hicho kiwe kitovu cha kuzalisha malighafi mbalimbali badala ya kuagiza nje ya Mkoa.
"Tunataka Don bosco shindani ambayo itakuwa na Kampuni tanzu ya kufanya shughuli nyingi unakuta mafundi wazuri wanatoka dar tunataka vijana wakitoka hapa chuoni wawe chachu kwenye Jamii wakienda kwenye Kampuni wanaaminika na kwenda kufanya Kazi kwenye majengo makubwa "
"Lazima
muwe na uso wa kazi mfungue Kampuni zitakazo husiana na fani zenu mnazofundisha
mtapata masoko ,tenda nyingi na kuongeza kipato cha chuo na taifa kwa
ujumla huku tukiangalie namna ya kusapoti vijana wenye ujuzi lakini hawana
uwezo " amesema Mtaka.
Aidha amesema kuwa chuo kimekuwa kikiwasaidia vijana kitaaluma kwa kuwatafutia ajira ,kukuza karama michezo,mziki kuwakuza kimalezi na kiimani huku wakipata elimu ya ziada.
"Tumejenga Mahusiano mazuri Kati ya vyuo vya ufundi stadi (VETA),kwa kuwaunganisha wanachuo kupitia soko la ajira, kuzalisha umeme wa solar ambapo tuna kilowatt 34 na kusaidia chuo kupunguza gharama za umeme,na tumeanzisha fani ya kilimo ili kuwasaidia vijana wasiwe legelege na kukuza kiwango cha kujitegemea Katika kilimo."amesema Padri Chami
Padri Chami amesema kuwa licha ya mafanikio hayo Bado Kuna changamoto ya mila na desturi mbovu kwa jamii juu mtoto wa kike kusomea fani za ufundi kwa madai kuwa ni kazi ya wanaume na kupelekea wazazi kutowajibika ipasavyo
Hata
hivyo amesema chuo kina mkakati wa kujenga mabweni ya wasichana ambayo watalala
hapo ili wapate muda wa kujisomea.
0 Comments