📌RHODA SIMBA.
MKUU wa
Mkoa wa Dodoma Anthon Mtaka amelitaka shirikisho la vyama vya
wafanyakazi nchini (TUCTA) kutokuwa na migongano,migawanyiko, na
migogoro katika vyama kwani watakosa kauli ya pamoja ya kutetea maslahi ya
wanachama wao.
Kadhalika amesema
Vyama vya wafanyakazi vina mchango mkubwa kwenye matokeo yanayoonekana hasa
kwenye kupanda madaraja,uboreshwaji wa maslahi ya wafanyakazi na
makundi mengine ya ajira katika siku za hivi
karibuni yameonekana kupata muafaka.
Ameyasema hayo leo
Novemba 11 jijini hapa wakati akifungua mkutano mkuu wa saba wa kuchagua
viongozi watakaohudumu kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025,Mtaka
amesema maelewano ndani ya shirikisho hilo ndiyo ngao kuu.
“Nyinyi ni vyama vya
wafanyakazi uchaguzi una mambo mengi lakini kwenye
mwamvuli huo wa mambo mengi lazima mjitambue mkiingia kwenye
hiyo migongano mgawanyiko na migogoro mtakosa kauli ya
kuisema serikali kwasababu kama nyinyi wenyewe mnapalangana mnafitishiana mnasemeana
mambo mabaya hamtafika,
Lazima muwe na mshikamano kama nyinyi wenyewe siyo taswira hamtafika Wanachama mnatakiwa muhubiri haki umoja ndani ya vyama vyenu mnao umoja mkikaribisha mambo ya ovyo kwaajili ya uchaguzi wa siku moja mtapotea
“Niwaombe uchaguzi wa
kesho kazi ya siku moja isiwakosanishe we omba kura tu, mtachafuana lakini
mwisho wa siku lazima kiongozi apatikane ogopeni teknolojia msijitoe kwenye
maisha ya kuwa viongozi kwajili ya mambo ya ovyo maana leo mtajibizana camera
zitahifadhi mwisho wa siku unaanza kusambazwa mitandaoni”amesema Mtaka.
Aidhaa mesema maana ya kutafuta kiongozi ni kutafuta mtu ambae anaweza kukaa na kutetea wanachama wake na kuzungumzia masilahi,na changamoto za wanachama.
Awali akisoma
risala kwa kwa mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu TUCTA Said Wamba
amesema Mkutano huu ni wa saba unachagua viongozi
utakaoongoza mpaka 2025.
Amesema kama
shirikisho wanafanyia kazi na kusimamia katiba na kutetea
vijana kama kauli mbiu inavyo ashiria na kupigania haki ya vijana
kupata ajira ya elimu na ujasiriamali.
Wamba amesema kumekuwa
na changamoto ya baadhi ya waajiri kuwazuia wafanyakazi kutojiunga na vyama
hivyo kitu ambacho si haki na ni kumnyima uhuru mfanyakazi hata
hivyo shirikisho hilo lina wajibu wa kusimamia Haki, wajibu na
umuhimu wa mshikamano na kudumisha uhusiano mwema katika kazi
na kutetea ajira.
“Takwimu za kila
mwaka zinazotolewa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali
zinabainisha kuonekana kwa ongezeko kubwa la ukosefu wa
ajira nchini na hasa kwa vijana.
Takwimu zinaonesha
idadi ya ajira inaonesha imezidiwa na idadi ya vijana wanaohitaji.
“Tunashukuru
kwasababu vijana wanajiongeza wanafanya ujasiriamali ingawa bado
hatuna jinsi ya kuwawezesha mipango yote ya serikali imeonesha mipango mbali
mbali, shirikisho linatambua kuwa watu wote hawawezi kupata kazi Serikali “
Kwa upande wake Rais
wa shirikisho hilo Tumaini Nyamhokya amesema msimamo wao ni
kuendelea kutetea wafanyakazi na kulinda mali za shirikisho nakuwaongezea
thamani wafanyakazi.
Nafasi zitakazogombewa
katika uchaguzi huo ni; Rais, Makamu wa Rais,Katibu,Naibu Katibu
mweka Hazina ,Wadhamini.
Wengine ni Mwenyekiti kamati ya wanawake, Makamu mwenyekiti wanawake, pamoja na kamati ya wanawake.
Mkutano huo wa uchaguzi umebebwa
na kauli mbiu isemayo ‘kazi ajira na maendeleo ya wafanyakazi’.
0 Comments