Muwasilishaji mada kutoka MISA TAN Jesse Kwayu akiwasilisha mada mbele ya kamati ya Bunge ya Miundombinu |
📌NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika(MISA) tawi la Tanzania imeomba kamati ya Kudumu ya
Bunge kuangalia na kuomba kupitia upya kwa baadhi ya vifungu katika sheria ya
Huduma ya Habari (MSA) ya mwaka 2016.
Akizungumza katika kikao kazi kati ya viongozi wa
MISA-Tanzania na Kamati hiyo,Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Andrew Marawiti
amesema wameamua kuishirikisha kamati hiyo kutokana na wajibu wa kamati hiyo
katika mambo ya habari.
Marawiti amebainisha kuwa iwapo baadhi ya vifungu vya sheria
hiyo vitaanza kutumika kwa kiasi fulani vitanyima uhuru wa upatikanaji wa
habari nchini.
Licha ya katiba na sera kuwepo,bado kumekuwa na changamoto mbalimbali za mfumo wa sheria zetu za nchi kuonekana kuna baadhi ya vifungu ambavyo sio rafiki kwa vyombo vya habari na vinaminya uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uhuru wa kujieleza.
Marawiti
Amesema kutokana na sekta ya habari nchini Tanzania kuwa
moja ya sekta muhimu kwenye kuchochea maendeleo ya taifa wameamua kuishirikisha kamati hiyo ili kusaidia
kufikisha ujumbe Bungeni ili kuangalia upya sheria hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Anne-Kilango Marcela akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kamati na viongozi wa MISA TANZANIA. |
“Leo kama mnavyojua muda mchache ujao tutaenda kumsikiliza
waziri Mkuu,ninacho waomba muandae kikao na kamati hiii lakini mje mkiwa na
maelezo ya kina kuhusu vifungu hivyo na madhara yake,lakini pia mje na
mapendekezo mnataka iweje?” amesema Mheshimiwa Anne Kilango.
Wabunge wakichangia maoni yao wakati wa kikao hicho. |
Naye Michael Gwimile (Muweka hazina-MISA TAN) ambaye
alimuakilisha Mwenyekiti wa MISA TAN amesema wamechukua ushauri huo wa kamati
na kuahidi kutekeleza yale yote waliyoshauriwa kwa ajili ya kikao kijacho kama
ilivyopendekezwa na kamati hiyo.
Licha ya Sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka
2016,sheria nyingine ambazo wadau wa habari wanazipigia kelele na kuomba
kupitiwa upya kwa baadhi ya vipengele katika sheria hizo ni; sheria ya makosa
ya kimtandao ya mwaka 2016 na sheria ya takwimu ya mwaka 2016.
Pia kuna kanuni mbalimbali ikiwemo kanuni za sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2017, kanuni za maudhui ya mitandao ya mwaka 2018,wadau wa habari wanazitaja kanuni hizo kuathiri mwenendo wa vyombo vya habari nchini.
0 Comments