Kamishna wa Operasheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Liberatus Sabas anatarajiwa kufunga mafunzo ya medani za kivita kwa maafisa wa jeshi hilo katika kambi ya Mkomazi mkoani Tanga.
Kamishana Sabas atafunga kozi hiyo hapo kesho (27/11/2021) ikiwa ni wiki ya mbili tangu kuanza kwa mafunzo hayo yaliyojumuisha maafisa wa Polisi 749 kuanzia tarehe 13/11/2021.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na chuo cha taaluma ya Polisi cha
Dar Salaam(DSM Police Academy) na
yalianza rasmi tarehe 18 June katika hatua za awali kabla ya kuhamia
Mkomazi kwa mafunzo ya medani.
Mkuu wa Chuo cha Taalum ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
akiongea na wanafunzi wa kozi ya Uofisa baada ya kukagua maandalizi ya sherehe
za kufunga mafunzo hayo katika Kambi ya mafunzo ya medani za kivita Mkomazi
mkoani Tanga.
Aliyesimama nyuma ni Mkufunzi mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, ACP Lutusyo Mwakyusa. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa kesho
0 Comments