WITO WATOLEWA KUPUNGUZA WAFUNGWA GEREZANI

 

Na,Mwandishi wetu-Dodoma

IMEELEZWA kuwa ipo haja kwa  mahakama kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani kwani idadi ya mahabusu imekuwa ni kubwa kuliko wafungwa.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Neema Rugangira amesema  mapaka hivi sasa kuna takribani mahabusu 17,000 huku wafungwa wakiwa ni 14,000 hivyo idadi ya mahabusu imekuwa ni kubwa zaidi ya wafungwa

Rugangira ameyasema Octoba 28  jijini Dodoma katika maonyesho ya wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI katika mdajadala wa haki jinai uliolenga kuangazia makosa yasiyo na dhamana haki ya dhamana kwenye makosa yasiyodhaminiwa.

Mbali na hayo Mbunge huyo  amesema kuwa njia pekee ya kusaidia hili ni kupunguza idadi ya mahabusu  na  ukitazama makosa ya mahabusu asilimia ya mahabusu ni watu wenye makosa yenye dhamana ‘’Nitumie fursa hii kuwaomba Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC mfanye tafiti kwenye makosa yenye dhamana’’

Ameongeza kuwa  mara zote anapoibua mijadala ya namna hiyo ndani ya Bunge amekuwa akipata ushirikiano ‘’Nadhani  wengi mtakubalina nami Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameshasema mara kadhaa kuhusiana na suala la uchelewashaji wa kutoa hukumu,msongamano mkubwa gerezani na hata mara ya mwisho alitoa maelekezo yake kuwa angependa kuona tunapunguza msongamano mkubwa gerezani ‘’

Post a Comment

0 Comments