Na Josephine Mtweve,
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge amewataka wananchi kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) ili kupata ushauri wa kisheria, kujua kazi wanazofanya na kusherehekea kwa pamoja mchango wa AZAKI kwa maendeleo ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mahange amesema uzinduzi utafanyika tarehe 23 oktoba ambapo utatanguliwa na matembezi ya amani ya Asasi za Kiraia yatakayoanza saa moja asubuhi.
Amesema ufunguzi huo utahudhuriwa na mgeni rasmi mheshimiwa spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini wakiwemo wananchi, serikali na sekta binafsi.
"Matembezi yataanzia kwenye shule ya sekondari Dodoma Hadi uwanja wa jakaya kikwete na baada ya ufunguzi huu maonyesho ya kazi za AZAKI yataanza,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda amewataja Viongozi na wageni mbalimbali kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pmaoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.
“Katika kusherehekea mafanikio ya sekta ya AZAKI na ubia Wetu baina ya wananchi maonyesho yatakayofanyika tarehe 23 hadi 24 Oktoba Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Profesa Jay,Sheta,Barnabas,Gnako,na wasanii wa Dodoma,”amesema.
Kaulimbiu ya AZAKI kwa mwaka huu ni mchango wa Asasi za Kiraia katika maendeleo ya nchi yaani AZAKI NA MAENDELEO.
0 Comments