Na Zainabu Mtoi, Agness Peter,
MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Matiafa(UN) Nchini Tanzania,Bw. Zlatan Milisic, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchangia walinda Amani wa Umoja wa Matiafa
Akizungumza jijini Dodoma katika siku ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Matiafa Milisic ameendelea kusisitiza ushirikiano wa muda mrefu kati ya Serikali na watu wa Tanzania, washiriki wa kimaendeleo wakimataifa na Umoja wa Matiafa ili kufikia lengo la maendeleo endelevu.
Amesema ujumbe Mkuu wa mwaka huu katika siku ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Matiafa (UN) ni kujijenga tena kwa kuweka mifumo bora ya Afya pamoja na malengo muhimu ya dunia ya kufikia lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) la 3: Afya bora na Maendeleo kwa Taifa.
"Hatuna budi kuendelea kushirikiana kuunga mkono juhudi zote za kujenga mifumo ya Afya iliyo na uhimilivu zaidi itakayo hakikisha jamii na watu wanakuwa na Afya bora, wanapata huduma za msingi za Afya na wanaweza kuhimili majanga ya kiafya kama UVIKO-19"amesema.
Amesema tangu janga hilo la UVIKO-19 litangazwe kuingia nchini Tanzania, Umoja wa Matiafa wamekuwa mstari wa mbele kusaidia nguzo mbalimbali katika mwitikio wa kitaifa dhidi ya janga hilo ambapo baadhi ya mashirika na Umoja wa Matiafa yakishika uwenyekiti wenza wa nguzo hizo za mwitikio.
Aidha Bw. Milisic amesema kutokana na mwitikio huo Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishirikiana na washirika wa kitaifa na kimataifa katika kuhakikisha kuwa huduma muhimu za Afya kama vile za akina mama, watoto na vijana balehe,VVU/UKIMWI na ukatili wa kijinsia zinaendelea katika kipindi chote cha janga.
Amesema misaada yao ya mifumo ya Afya hukuanza katika zama la janga la UVIKO-19 tu, kwa miaka mingi Umoja wa Matiafa wamekuwa wakichangia katika kuimarisha mifumo ya Afya kwa kusaidia, kujenga, kurekebisha na kuvipa vifaa vituo vya Afya.
"Tumekuwa tukijenga na kufanya marekebisho ya kliniki na zahanati, baadhi zikiwa pembezoni mwa nchi na kuvipa vifaa vinavyohitajika ili kuhakikisha wanawake wanapata pahala pa kujifungulia kwa usalama na watoto wao wachanga wanapata matunzo yanayostahili"amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Matiafa Antonio Gutteres amewaomba watanzania kuungana pamoja kukabiliana na changamoto na kuendeleza malengo ya Maendeleo Endelevu.
Amesema wanapoadhimisha siku ya Umoja wa Matiafa, waungane wote kwa pamoja katika kuunga mkono tunu hizo wakiishi ile ahadi kamili, uwezekano na matumaini ya Umoja wa Matiafa.
0 Comments