SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUJA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI KAMPENI YA MAENDELEO YA TAIFA DHIDI YA UVIKO 19



 Na Saida Issa,Dodoma.

SERILAKI kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imeanza utekelezaji wa kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 katika kujenga miradi  kwa kutumia fedha za mkopo wenye masharti nafuu zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wenye thamani ya shilingi Trilioni 1.3 huku lengo la miradi hiyo likiwa   ni kuboresha huduma za afya kwa 

Hayo yameelezwa jijini hapa leo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari Habari.saa sita kamili katibu mkuu ataongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa fedha za uviko yenye  malengo ya miradi inayotekelezwa chini ya Wizara yake ili kuimarisha huduma za dharura, wagonjwa mahututi na wanaohitaji uangalizi maalum .

“Uwekezaji huu unategemewa kupunguza vifo vya wagonjwa kwa asilimia 20-40  ndani ya vituo vya afya, utaimarisha huduma za maabara, mionzi na tiba mtandao ambapo  itasaidia ugunduzi wa haraka wa magonjwa mbalimbali na kupunguza rufaa"ameeleza

Pia amesema,uwekezaji wa miradi hiyo pia itasaidia kuimarisha huduma za chanjo dhidi ya UVIKO - 19 na elimu ya afya kwa umma dhidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo,kuimarisha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za Afya,kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Korona pamoja na kuwajenga uwezo watoa huduma za Afya

Amesema,tayari wizara yake imeanza ukarabati na kujenga majengo ya matibabu ya dharura (EMD) 102, vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangallizi maalum (ICU) 67 na kusimika vifaa vyake,kuimarisha mfumo wa rufaa kwa kununua na kusambaza magari 253 ya kubebea wagonjwa’Advanced ambulance’ ambapo  kati ya magari hayo magari 20 yatapelekwa katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere, KIA , Mwanza , Hospitali ya Mzena, Hospitali za Rufaa za Mikoa minane, Hospitali za Kanda sita, Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi.

Amesema kati ya magari hayo , 233 ni ya kawaida ‘basic ambulances’ na yatapelekwa Hospitali za Rufaa za Mikoa 38 na magari 185 katika ngazi ya ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo,uwekezaji huo katika sekta ya Afya utaimarisha  upatikanaji wa damu salama kwa kununua kusambaza vifaa nane vya kisasa vya kukusanyia damu ‘mobile blood collection vans’ katika  Kanda ya Ziwa - Mwanza Kanda ya Mashariki - Dar es Salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini-Mbeya,Kanda ya Kusini – Mtwara, Kanda ya kaskazini – Kilimanjaro, Kanda ya Magharibi – Tabora, Kanda ya Kati – Dodoma, Kanda Maalum ya Jeshi na ofisi za Makao Makuu Dar Es Salaam.

“Pia uwekezaji huu utaimarisha upatikanaji wa hewa tiba ya oksijeni kwa kununua mitambo 10 ya kuzalisha hewa hiyo na kuisimika kwenye vituo vya kimkakati vya kutolea huduma za afya zikiwemo vituo vilivyo mbali na hospitali za mikoa iliyosimikwa mitambo tayari na vile vyenye idadi kubwa wagonjwa,utawezesha huduma za upasuaji kwa kununua na kusambaza mashine 60 za kutolea dawa za usingizi na ganzi pamoja na vifaa vingine muhimy vya vyumba vya upasuaji  katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha amesema,katika eneo la kuimarisha huduma za kimabaara na mionzi na tiba mtandao,wizara imepanga kuimarisha uwezo wa  Maabara ya Taifa na Maabara nyingine nchini ili kupima na kutoa majibu ya sampuli kwa wakati lakini pia vitanunuliwa na kusambazwa vitendanishi vya kupima sampuli katika maabara za mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Dodoma, Arusha (Mt. Meru), Tanga na Mtwara .

Pia wizara katika eneo hilo wizara itaimarisha huduma za uchunguzi wa mionzi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hizo wakiwemo magonjwa wa kansa, moyo, kifua kikuu na mifupa lakini pia  itanunua na kusimika mashine 95 za X – Ray za kidigitali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili , Hospitali ya Kanda Chato  na Mtwara , Hospitali za Rufaa za Mikoa 20 na X – Ray 70 zitasimamiwa na OR TAMISEMI.

Pia, sekta itanunua na kusimika CT – Scan 29 ambapo, Hospitali ya Taifa Muhimbili , Hospitali za Kanda ya Chato na Mtwara , Hospitali ya Jeshi Lugalo, hospitali ya Uhuru  na Hospitali 24 za Rufaa za Mikoa.

Aidha amesema,mashine nne a MRI zitanunuliwa na kusimikwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali za Kanda ya Mtwara, Hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean na Hospitali ya Kanda Chato  lakini pia Serikali itanunua mashine saba za huduma za uchunguzi wa moyo (Portable Echo Cardiography) kwa ajili ya Hospitali za Kanda sita pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

“Vile vile, sekta inaimarisha huduma za tiba mtandao (Telemedicine) kwa kukarabati na kuweka vifaa katika vitovu maalum vya Huduma ya Tiba Mtandao (Telelmedicine Hubs) Kwenye Taasisi nne za Rufaa za Ubingwa Bobezi ambazo ni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, na Taasisi za Kanda ya Ziwa Bugando na Benjamin Mkapa Dodoma. Vilevile katika hospitali zote za Rufaa za Mikoa kutafanyika ukarabati wa vyumba maalum vya Huduma ya Tiba Mtandao (Regional Telelmedicine centre Rooms) ambavyo vitaunganishwa kwa njia ya Mtandao na Vitovu (Hubs) zilizoko kwenye Hospitali za Rufaa za Kanda na zile zilizoko kwenye Hospitali Maalumu za Ubingwa Bobezi. “amesema

Kuhusu kuimarisha na kuhamasisha jamii kupata chanjo dhidi ya UVIKO - 19 pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo profesa Makubi alisema,Sekta ya Afya inaimarisha upatikanaji wa huduma za chanjo ya UVIKO – 19 kwa kugomboa, kutunza na kusambaza takribani dozi milioni 1.16.

Kwa mujibu wa Profesa Makubi pamoja na maelekezo ya Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma Sheria, Kanuni na miongozo ya manunuzi zitafuatwa ili kupata thamani ya fedha, ubora na viwango stahiki kwa miradi itakayotekelezwa chini ya sekta ya afya.

Profesa Makubi alisisitiza katika eneo la usimamizi na ufuatiliaji huku akisema,Sekta ya afya imejipanga katika usimamizi, ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments