POSTA YADHAMIRIA KUONGEZA KASI YA UTOAJI HUDUMA KWA WATANZANIA


 

Na Josephine Mtweve, Zainabu Mtoi na Agness Peter,

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt.Jabir Kuwe Bakari amesema lengo la warsha ya watoa huduma za posta ni kuchochea kasi ya utoaji huduma ili wananchi ambao hawajafikiwa na Postikodi waweze kufikiwa ili kurahisisha upatikanaji w huduma

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Posta duniani jijini Dodoma Octoba 7 mwaka huu,Dkt.Bakari  amesema wao kama Mamlaka jukumu lao ni kuhakikisha taratibu za Postikodi zinakuwa sawa na zinazingatia taratibu za kimataifa ili mtoa huduma za kimataifa anapokuja Tanzania awe na uwezo wa kutoa huduma bila kupata changamoto yoyote.

Amesema wako na muelekeo mzuri kwani kwa kutumia Teknolojia wamepanga kuboresha changamoto ambazo sekta ya Posta ilikua nazo hapo nyuma.

''Tuko vizuri kwa sababu tumeona Teknolojia ilivyotumika kutengeneza mifumo ambapo sasa mambo ambayo nyuma yalikua vigumu kufanyika sasa yanafanyika,kwa mfano ununuzi wa vifaa ilikuwa ni lazima uende dukani au kwa mjasiriamali alietengeneza hicho kitu lakini hivi sasa kwa kutumia simu au Kompyuta yako huyo aliye tengeneza hiyo bidhaa ataweka pale kwenye duka la posta na mtumiaji ataweza kununua,’’Alisema.

Aidha Dkt.Bakari ameongeza kuwa katika wiki ya huduma kwa mteja,wamelenga kukaa na watoa huduma na wale wanaopokea huduma kuangalia utaratibu mzima wanavyotoa huduma na uzingatiaji wa masharti wakati wa utoaji huduma kwa njia ya Postikodi.

Naye Afisa Masoko Kitengo cha Huduma za Rejereja (DHL) Abdala Ally Sharifu amesema kwa upande wao wanafuraha kubwa ya kujiunga na shirika la posta Tanzania pamoja na mashirika mengine ya usafirishaji na yale yanayohusika na mawasiliano.

Sharifu amesema wamekua wakisafirisha mizigo ya wateja nchi takribani 250 na wanahuduma nyingi ambazo kwa sasa wanatarajia kuja na huduma mpya za mtandaoni ambapo mteja aliyeko Tanzania anaweza kuagiza bidhaa yake mahali popote pale duniani na DHL wanaweza kuichukua kutoka iliko na kuifikisaha Tanzania bila tatizo lolote na kwa haraka zaidi.

‘’Tunahukuru kwa muunganiko ambao tunaupata kutoka Posta na imeturahisishia sana kwa baadhi ya maeneo ambayo tulikua hatufiki kwa uharaka na kwa nafasi hii ambayo sisi tulikua tunataka tufike lakini kwasababu posta walikua wameshafika katika maeneo hayo basi ushirikiano wetu na Posta Tanzania umetusaidia sana kuwafikishia watanzania huduma hii,’’Alisema




Post a Comment

0 Comments