Na Agness Peter, Josephine Mtweve na Zainabu Mtoi,
MWENYEKITI wa Jumuiya ya maridhiano Mkoa wa Dodoma, Evance Lucas Chande ametoa pongezi kwa Mhe. Rais kwa kulibadilisha Taifa katika masuala ya kimataifa na kufanikisha kulishawishi shirika la fedha la kimataifa (IMF) kwa kulipatia taifa fedha kiasi cha shilingi Tilioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma, Askofu Chande amesema kiwango hicho cha fedha ni kikubwa hasa kwa kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na janga la UVICO-19.
Anampongeza Rais samia kwa namna alivyotoa maelekezo ya fedha hizo kwa matumizi ambayo yanalenga kumnufaisha mtu wa kipato cha chini.
"Fedha hizo zimeelekezwa kwenda kujenga shule ya msingi, madarasa ya sekondari, vifaa tiba na mitambo ya hospitali,hatua hiyo itakwenda kuimarisha sekta ya afya na ni muhimu sana hasa kwa kipindi hiki cha UVIKO-19 ambapo kulikuwa na upungufu wa mitungi ya gesi ya oksijeni na dawa''Alisema.
Aidha ameendelea kuipongeza kasi ya utendaji kazi wa Rais Samia kwenye suala la maji vijijini pia kwa kutenga fedha kwa ajili ya kununua mitambo ya kuchimba visima vijijini.
Amesema tatizo la maji vijijini ni kubwa na gharama za kuchimba visima ni kubwa na anaamini kuwa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima litaenda sambamba na upatikanaji wa maji kwaajili ya kilimo cha mbogamboga vijijini na wanatambua maji safi yakipatikana yanaleta afya kwa wanakijiji na kupunguza magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
"Watanzania wengi kwa sasa tunamuelewa Mhe.Rais, ni kwelii kama anavyosema amevaa viatu vya Hayati Magufuli japokuwa anasema ni vikubwa, lakini sisi tunaona havijampwaya, viatu hivi ni saizi yake na hatua tu kwani hata aliyoyafanya JPM hakufanya mara moja, alifanya kwa miaka mitano, "alisema.
Aidha Askofu Chande amewaomba watendaji wa Rais wasimwangushe, wachape kazi kwa bidii ili Tanzania iwe na maendeleo ya kutosha.
0 Comments