MAASKOFU NA WACHUNGAJI WATAKIWA KUIBUA MIRADI YA KIMKAKATI ITAKAYOWALETEA MAENDELEO.



 Na Agness Peter,

ASKOFU Mkuu wa kanisa la PHAM (T) Nkumbu Mwalyego amewataka  Maaskofu na Wachungaji ,kuibua miradi ya kimkakati itakayowaletea maendeleo kwa kufanya kazi za mikono kama vile kilimo,biashara na ufugaji ili waweze kujiinua kiuchumi na kiroho.

Ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la mwaka la Wachungaji Kitaifa (PHAM (T) miaka 10 ya Maongezeko yenye mguso lililofanyika mkoani Dodoma,ambapo amewaagiza kufanya kazi hizo ili kuleta matokeo  chanja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa,kanisa na wao wenyewe .

Mwalyego amesema kuwa badala ya kutegemea sadaka na asilimia za mafungu ya kumi,ni wakati sasa wa kufanya kazi kazi za mikono ili waweze kujiinua kimapato kwenye utumishi wao.

" Maaskofu na wachungaji wanatakiwa kuzitambua fursa zilizopo na walizonazo wao wenyewe kwenye nafasi ili kuifanya kazi ya Mungu ipasavyo ikiwa na kuibua miradi  ambayo itakayowabadilisha maisha yao ya kiroho na kimwili, " amesema.

Pia amewataka kuendelea kujiendeleza kielimu zaidi ili waweze kufanyaka kazi za kumtumikia Mungu kwa ufanisi wa kuleta maendeleo kwa ajili ya kanisa na Taifa ambao utakaolingana na mpango mkakati wa miaka hiyo kumi.

Amesema kuwa kuna ulazima wa kuifanya kazi ya kiroho kwa njia ya kisasa na kisomi zaidi,ili kuondokana na mazoea ambayo yaliyokuwa huko miaka ya nyuma.

Mwalyego amesema wanatakiwa kujipima wao wenyewe kwenye utendaji ili waweze kujitambua na kuleta mabadiliko yatakayowezesha kanisa kuhubiri kwa njia za kisasa na hatimaye kuongeza waumini kila upande wa nchi.

Post a Comment

0 Comments