📌ANGELA MSIMBIRA (TAMISEMI)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameielekeza Tume ya Utumishi wa waalimu
nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa
waalinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
ili kuweka uwiano sawa wa waalimu nchini.
Akiongea na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa
waalimu Jijini Dodoma Waziri Ummy amaesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa
baadhi ya shule kuwa na waalimu wengi huku nyingine zikikosa waalimu,
hivyo ni wajibu wa tume kuhakikisha
suala hilo linashughulikiwa kwa wakati
Waziri Ummy amesema kuna baadhi ya shule zina watoto wengi lakini waalimu ni wachache huku shule nyingine zikiwa na waalimu wengi wanafunzi wachache, ni vyema kukawa na uwiano ulio sawa katika shule zote nchini.
Tunafahamu kuwa zipo shule ambazo zina waalimu wachache hasa maeneo ya vijijini, lakini nyingine zinawaalimu wengi, suala hili halikubaliki, suala hili linahitajika kufanyiwa kazi ingawa mara nyingi serikali inaangalia idadi ya wanafunzi
Waziri Ummy ameendelea kueleza kuwa kutokufanya msawazo hatuwatendei haki wanafunzi walioko vijijini hasa katika maeneo ya pembezoni ni wajibu wa tume kuhakikisha shule zote zinakuwa na idadi sawa ya waalimu
Aidha amewaelekeza Tume ya Utumishi wa Waalimu
nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kutatua kero za waalimu nchini
ili kupunguza changamoto hizo kwa haraka na kutoa mrejesho kwa waalimu kwa
wakati
0 Comments