📌AGNESS PETER,DOMECO
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Dkt.Dorothy Gwajima, amekipongeza Chama Cha Wataalamu wa Epidemioljia na
Maabara kwa kuanzisha siku ya
maadhimisho ya wataalamu wa epidemiolojia na maabara duniani.
Akizungumza na wawakilishi, wananchi na waandishi wa habari
leo jijini dodoma, Gwajima amesema anafahamu kwamba ni mara ya kwanza nchini
kuadhimisha siku ya wanaepidemiolojia na maabara ambayo kimsingi ni wadadisi wa
magonjwa ya kuambukizwa na ambayo sio ya kuambukizwa (Diseases Detective)
Amesema anaamini Shirika la Afya Duniani (WHO) litakubali na
kuweka muongozo katika kalenda za shirika lake kwamba siku ya tarehe 07 Septemba
itakuwa siku ya maadhimisho hayo na watasubiri muongozo huo .
Ujumbe wa maadhimisho haya kwa mwaka huu ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa matukio ya kiafya ili kubaini haraka matishio ya kiafya katika jamii.
‘’ Nawapongeza
wataalamu wote wa epidemiolojia na maabara hapa nchini ambao wengi wao ni
wahitimu wa programu ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na
watoto inayoratibu mafunzo ya kiepidemiolojia na udhibiti wa magonjwa hapa
nchini kwa kushirikiana na chuo kikuu
cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili,’’amesema.
Amesema utekelezaji wa programu hiyo nchini ni jukumu la Wizara
ya Afya kwa kushirikiana na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi(MUAS)
lengo ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa afya ya jamii kwa kuboresha uwezo
wa kupunguza upungufu wa wataalamu wa kiepidemiolojia na udhibiti wa magonjwa
ya chini.
Dkt.Gwajima amesema mafunzo yanatolewa kwa muda wa miezi
mitatu au muda wa kati miezi sita kwa kupata cheti au kukaa miaka miwili na kupata shahada ya
uzamifu wa masuala ya sayansi na epidemiolojia, udhibiti wa magonjwa na masuala ya maabara.
Amesema mafunzo hayo yanatarajia kutoa wataalamu wa
epidemiolojia na sio tu katika afya ya
binadamu bali pia katika afya ya wanyama na wataalamu hao watakua na ujuzi wa
afya na ufanisi katika ngazi ya jamii na kuweza kutambua magonjwa ya milipuko
na matukio mengine yenye hatari za kiafya kwa haraka na kutoa taarifa katika ngazi ya jamii na
wizarani ili yaweze kudhibitiwa kwa wakati.
‘’Wengi watajiuliza hapa kwanini kuna uhusino wa kujifunza kozi hii kwa wanyama na binadamu, ndiyo kwasababu sisi tunaishi na wanyama na wanaweza kutengeneza magonjwa alafu sisi kama hatuna wataalamu hawa wa kuweza kupima nyama inayoenda sokoni tunaweza kukuta tumebeba magonjwa ya wanyama tukaanza kuugua." amebainisha Waziri Gwajima.
Pia Waziri huyo amesema matumizi ya takwimu zenye ubora katika
ngazi za chini ili kuweza kufanya maamuzi yenye ushahidi wa sayansi bado ni changamoto katika
halmashauri.
0 Comments