📌ANGELA
MSIMBIRA (TAMISEMI)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali Mhe Ummy Mwalimu amesema walimu
wanaotaka kuhama kutoka mijini kwenda
vijijini ni ruksa, lakini
wanaohamishwa kutoka vijijijini
kwenda mjini tume ya utumishi wa walimu nchini ihakikishe kabla ya kuwahamisha wawe na walimu mbadala.
Akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi Tawi la
Tume ya Utumishi wa Walimu leo Jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa ni
marufuku kuhamisha walimu kutoka katika Halmashauri zilizoko pembezoni kabla ya
kupeleka waalimu mbadala
Amesema kuwa uhamisho ni haki ya mtumishi lakini
changamoto kubwa wengi wanataka kuhama kutoka Halmashauri za vijijini kwenda
mijini, hili haliwezekani, lakini kama amekaa zaidia miaka mitatu na anahitaji
kuhama ihakikishwe kunakuwepo na walimu mbadala wa kuziba nafasi inayoachwa na
mwalimu anayehama.
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imejikita katika
kutoa elimu bora kwa jamii kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora ya
kufundisha na kujifunzia ni wajibu wa tume sasa kuhakikisha uwiano wa walimu
unafanyika ili kutoa elimu sawa kwa watoto wote wa Kitanzania hasa katika Halmashauri
zilizopo pembezoni.
Aidha
Aidha,ameitaka tume ya Utumishi wa Walimu kufanya tathmini ya kina kwa kuangalia uwiano wa waalimu kwenye shule za Msingi na Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa lengo likiwa ni kuwa na takwimu sahihi za mahitaji halisi ya walimu na uwiano uliosawa katika Halmashauri.
0 Comments