📌JOSEPHINE MTWEVE, DOMECO
KATIBU Mkuu wa Chama chaVisiwi mkoa wa Dodoma Amina
Issa amewataka waandishi wa habari kusoma Lugha ya alama ili kusaidia kundi
hilo kushirika katika mijadala itakayosaidia kutatua changamoto katika jamii.
Akizungumza ofisini
kwake jijini Dodoma Bi.Amina amesema kumekuwa na changamoto za upatikanaji wa
habari kwa viziwi na mambo kama hayo lazima waelezwe waandishi wa habari ili
changamoto zao zitatuliwe.
Amesema ameona
ni vizuri kukutana na waandishi wa habari ili kuweza kuona kwa namna gani
wanaweza kuwa washirika wa karibu katika swala zima la kutatua changamoto
zinazokabili kundi hilo.
Ni jambo zuri kwa waaandishi kujifunza lugha ya alama , mfano ukienda Morogoro kuna baadhi ya waandishi angalau wanafahamu lugha ya alama ya msingi lakini kwa hapa makao makuu hakuna na ndiyo maana tunataka kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kufanikisha.
Amesema katika
mkoa wa Dodoma kuna viziwi zaidi ya 2000 kutokana na sensa ya mwaka 2012 na
wanachama walio hai ni katika umoja wao ni 642 kimkoa na wanachama wasio hai
takwimu zao hupatikana kutoka mashuleni pamoja na makanisani.
Bi Amina
amewaomba watu wenye matatizo ya usikivu kujitokeza na kujiunga na chama chao
hili waweze kupatiwa misaada mbalimbali ikiwemo mafunzo ya lugha ya alama
ambayo uratibiwa mara kwa mara.
Aidha mtafsiri wa lugha ya alama Adrian Chiyenje amesema kwa sasa kuna ongezeko kubwa la viziwi hasa mtaani kwa watu wazima na wanaonekana kukata tamaa.
Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma (CPC) Ben Bago amesema visiwi wapo kwenye jamii lakini sauti zao (maoni) hazisikiki hivyo lazima kuwe na umuhimu wa waandishi wa habari kujua lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano.
Bago amesema waandishi
wamekuwa wakifanya mahojiano na watu tofautitofauti lakini mara kadhaa lakini
hawawapi nafasi visiwi kutokana na changamoto ya mawasiliano.
Katibu huyo
ameahidi ushirikiano na chama hicho cha visiwi katika kuhakikisha waandishi mkoani
Dodoma wanajifunza lugha ya alama ili kuwawezesha kuandika habari zinazohusu
kundi hilo.
0 Comments