📌JOSEPHINE MTWEVE
NA ZAINABU MTOI
VIJANA
wametakiwa kutumia nguvu kazi zao kwa
kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kijamii badala ya kukaa vijiweni na
kuinyoshea vidole serikali.
Ushauri huo
umetolewa na Shekhe wa kata ya Chang’ombe Ibrahimu Kidura alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari baada ya
kushiriki dua na ujenzi wa msikiti wa kisasa wa Mccadam uliopo katika kata ya Chang’ombe
jijini Dodoma.
Shekhe Kidura
amewataka vijana kuhakikisha wanatumia nguvu
walizokuanazo kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ujenzi
wa nyumba za ibada.
Vijana ndiyo wenye nguvu na wanaweza kushiriki kikamilifu shughuli mbalimbali za kimaendelea ikiwemo na ujenzi, hivyo nawaomba vijana wajitokeze kwa wingi pale shughuli hizo zinapojitokeza
Naye Shekhe
Hussein Jumbe amewataka waumini wa dini ya kiislamu kata ya Changombe kuonyesha
mfano wa kuchangia mali na fedha kwaajili ya ujenzi wa msikiti badala ya
kutegemea watu wa nje na eneo hilo.
Shekhe Jumbe
amesema waumini wa kata hiyo wana wajibu mkubwa wa kuonyesha mfano katika
kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati kutokana na michango yao
watakavyojitoa.
Ninawaomba
waumini wa kata hii kujitokeza kwa wingi katika kushiriki ujenzi huu wa msikiti
ili uweze kukamilika kwa wakati
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Wilaya ya Dodoma (BAKWATA)
Bashiru Omari amewaomba waumini kutumia nguvu kazi zao ili kupunguza matumizi
ya fedha.
Bashiru amesema
kuwa wakitumia nguvu kazi na kujitoa kwa wingi ujenzi huo utaweza kukamilika
kwa wakati.
0 Comments