📌GIMU GALAFONI
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge,Vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema licha ya Serikali na Wadau mbalimbali kuwekeza nguvu kubwa kupambana na matumizi ya Dawa za kulevya suala la unyanyapaa kwa vijana wanaotumia dawa hizo linaonesha kudhorotesha juhudi hizo na kufanya matumizi ya Dawa kutokwisha.
Waziri Mhagama amesema hayo wakati akifungua kikao cha kamati ya bunge ya kudumu ya masuala ya ukimwi na Asasi za kiraia zinazoshirikiana na mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya jijini Dodoma.
Amesema jamii imekuwa inawanyanyapaaa watu wanaotoka kwenye Janga la Dawa za kulevya licha ya kuwa wameacha kutumia Dawa hizo hali hiyo inawapelekea watu hao kurejea kwenye matumizi ya Dawa kutokana na kukosa upendo na ushirikiano kwa jamii inayowazunguka hivyo ni vyema kuendelea kuelimisha jamii .
Aidha waziri Mhagama
amesema asilimia kubwa ya watumiaji wa dawa hizo ni vijana ambao ni
asilimia 56 ya nguvu kazi ya Tanzania hivyo ni vyema mamlaka
inayohusika na usimamizi wa dawa hizo kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na
wabunge ilikuwasaidia vijana hao huku akibainisha juhudi kubwa zilizofanywa na
mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) . Patrobas Katambi amesema pana uhitaji mkubwa wa kupata maarifa pamoja kuongeza tafiti zaidi huku Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Ummy Nderiananga akiahidi kushikiriana na wadau wa mapambano dawa za kulevya.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Fatma Taufiq amesema wao
kama kamati watajitahidi kuhakikisha bajeti inaongezwa katika kupambana na dawa
za kulevya huku kamishna wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana dawa za kulevya (DCEA)Gerald Kusaya amesema wamekuwa wakiwawezesha kiuchumi watu walioathirika
na dawa za kulevya.
Msimamizi huduma za Afya kwa waraibu dawa za kulevya kutoka mkoani Arusha Jesca Temu amesema wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali kuwarejesha waraibu katika hali ya kawaida .
Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa afya ya akili na Mwanzilishi wa
Huduma za MAT hospitali ya Muhimbili Frank Masao amesema
asilimia 83.4 ya watu waliokuwa wanajidunga walikuwa na matatizo ya ini
ambapo Mbunge wa viti Maalum Dkt.Alice Kaijage akihimiza zaidi kuongeza mfuko
wa kutosha kwa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya
0 Comments