UKICHANJWA UNAPATA TIKETI YA BURE KUANGALIA MECHI



 ðŸ“ŒMITANDAO

MASHABIKI wa mpira wa miguu wa nchini Afrika Kusini ambao wamepata chanjo wanaweza kupata tiketi ya kuingia bure kutazama timu ya Bafana Bafana ikicheza na Ethiopia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema.

Kiongozi wa Shirikisho la Soka la nchini humo (SAFA) Danny Jordaan mpango mpango huo utatumika kwa nusu ya tiketi zilizopngwa kwa ajili ya mechi.

Kulingana na mtandao wa  News24. Jordaan amesema hatua hiyo imetokana na makubaliano  na serikali na inategemea ni mashabiki wangapi wanaojitokeza, 

Serikali ina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa hisia za kupambana na chanjo nchini.

Watu milioni 10 tu wamechanjwa dhidi ya Covid-19, na serikali inasema malengo ni kuwafikia watu milioni 40 .

Lakini utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Ask Afrika uligundua kuwa ni 62% tu ya watu walikuwa tayari kuchanjwa - ikiwa ni chini kuliko lengo la serikali.

Ukosefu wa uaminifu na hofu juu ya athari-mbaya za muda mfupi au mrefu zilitajwa kama sababu kuu ya kuwafanya wananchi wa taifa hilo kutojitokeza kwenye chanjo.

Zaidi ya watu 80,000 wamekufa na Covid-19 nchini Afrika Kusini, zaidi ya nchi nyingine yoyote barani.

Vyombo vya habari vya vimemnukuu Bwana Jordaan akigusia umati wa watu unaoudhuria michezo mbalimbali barani Ulaya ikiwemo kwenye mechi za Euro 2020 mnamo Juni na Julai.

"Unapoangalia kile kinachotokea Ulaya, unaweza pata jibu kwa nini fainali za Euro zinaweza kuwa na zaidi ya watu 60,000 uwanjani, wanaweza kuwa na mashabiki wanaosherehekea kabla, wakati na baada ya mechi?"

Bwana Jordan alikuwa na ujumbe wazi kwa mashabiki ambao hawataki chanjo hiyo, kulingana na habari iliyochapishwa kwenye tovuti ya News24.

Ni wazi kabisa kwamba, ikiwa haujachanjwa, huwezi kuja uwanjani,Tunataka uje uwanjani. Hatutaki uende hospitalini.

Naye Naibu Rais wa nchi hiyo David Mabuza alisema tasnia ya michezo na sanaa ilihitaji hadhira kufanya kazi vizuri na "kuchangia kwa maana kwa uchumi".

Alisema lengo la kampeni hiyo ilikuwa kuhamasisha watu zaidi kupata chanjo ili waweze kuhudhuria viwanjani na hafla kubwa nchini humo.


SOMA HII PIA: WALIMU KUHAMA KUTOKA MIJINI KWENDE VIJIJINI RUKSA

Post a Comment

0 Comments