📌JOSEPHINE
MTWEVE
NAIBU
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoan na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI),Gerald Mweli, ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kufanya
tathimini ya upandishwaji wa madaraja uliokamilika hivi karibuni ili kubaini
masuala ya rushwa.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mafunzo ya kamati za walimu kutoka mikoa ya Dodoma, Iringa,
Singida na Manyara jijini Dodoma leo, Mweli amesema TAMISEMI imepokea
malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu
kwamba baadhi ya kamati za walimu katika ngazi za wilaya waliwapandisha
madaraja baadhi ya walimu wasiokuwa na
vigezo .
Amesema
tathimini inatakiwa ifanyika kwa haraka na kwa uwazi ili waweze kuchukua hatua
kwa baadhi ya kamati za wilaya ambazo
zilipandisha walimu madaraja kwa vigezo vya rushwa bila kuzingatia sifa za
walimu husika.
Tutakua makini na tutahakikisha haki inatendeka na hatutoacha kuwasaidia kufanya kazi zenu na kazi mojawapo ni kuwapa mafunzo
Aidha
amesema watahakikisha wanaanzisha kituo cha huduma kwa wateja ambapo kitawasaidia
walimu muda wowote kupiga simu kuwasilisha malalamiko, maoni na ushauri wao
endapo ushauri huo hautafanyiwa kazi katika ngazi za wilaya.
Naibu
katibu huyo amesema Tamisemi imeshaulipa mfumo huo, hivyo tume inatakiwa
kuwaandaa wataalamu na chumba maalumu kwaajili ya kupokea malalamiko ya walimu
na kuyafanyia kazi.
Mfumo huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi sita na uanze kufanya kazi ili kuwa na taarifa za ajira, nidhamu na mrejeshomwa rufaa zao
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Profesa
Willy Komba aliipongeza Tamisemi kupitia
kwa Naibu Katibu Mkuu (Elimu) kwa msaada wa kukwamua mambo mbalimbali
yakiwemo ya walimu kupandisha madaraja.
Profesa
Komba amesema anaiomba Tamisemi kuendelea kuwa bega kwa bega na Tume katika
kusaidia ajira za walimu, usafiri kwaajili ya walimu wilayani na makao makuu na
vifaa pamoja na vitendea kazi vyao.
Naye katibu
Mtendaji wa Tume, Paulina Nkwama amesema tume hiyo inaendesha mafunzo kwa
kamati za walimu za wilaya kwaajili ya kuwajengea uwezo wa kusaidia masuala ya
ajira ya walimu, nidhamu na maendeleo yao.
Amesema
wameshafanya mafunzo ya kujengea uwezo kamati kanda ya mashariki, kanda ya ziwa na
sasa wanafanya katika kanda ya kati , pia anaiomba Tamisemi kuiwezesha kifedha
tume ili ikamilishe katika kanda nne zilizobakia.
0 Comments